Mbunge kusimama Bungeni kutaka Rais aongezwe muda wa kukaa madarakani. Je, Umewasiliana na waliokutuma uwawakilishe hapo Bungeni au ni mawazo yako?

Hili halina mjadala mkitaka msitake Mheshimiwa Magufuli tunamuongezea mingine,sasa jamani mtu huyu hana kasoro kubwa sana za kiuongozi na imeonekanika kabisa sio hapa Tanzania tu,dunia nzima na ulimwengu wake hata huku kwenye ulimwengu wa tatu wananchi wa nchi nyingi wanawaonea gere wananchi wa Tanzania kwa kupata kiongozi mchapa kazi,kasoro ndogondogo ni za kiubinadamu ambazo hakuna anaeweza kuziepuka,kasoro hizo wazungu au mabeberu wanaziita minor yaani vitu viduchu viduchu,ambavyo haviathiri utendaji wake wa kazi.

Sasa wewe usietaka aendelee miaka mingine unataka utuletee mjomba wako ? na mkileta za kuleta tunaondoa hata uchaguzi kwani waTanzania hawana sababu ya kufanya uchaguzi kwa kuwa aliekuwepo anatosha,yanini kupoteza hela,ambazo zinaweza kutumika kuendeleza mfumuko wa miundo mbunu,

Sasa hivi WaTanzania tunahitaji Express train Mwanza tu Mtwara na hela ikitosha tunajenda ring road ya Tanzania nzima ikienda sambamba na reli, hii Ring road ndio mwisho ,sijui hawa wapinzani hewa kama wanelewa faida ya Ring road au wanaelewa ni kitu gani.
 
Kwani walichaguliwa lini kuwa wabunge?
 
Correction

Hakuna Mbunge aliyewahi “kuombwa” na wananchi awawakilishe. Wabunge ndio huomba na wananchi huwapa ridhaa.

Hii mentality ya Mbunge kuonekana ni hero au messiah flani ndo inatucost kama nchi.
 
Kwa asilimia kubwa Uongozi huu utaendelea kuwepo madarakani kama MUNGU atampa uhai na nguvu raisi. Ni vyema kujiandaa na kukubaliana na mtindo wa utawala esp kama ww ni kijana.
 
Hili ni swali zuri sana sana, hawa wabunge wanajua akiongezewa muda wake awatasaidia wapite tena kama walivyopita kwa magumashi basi hawana lingine maana wanaangalia matumbo yao wawe matajiri na wamisha yawe mazuri sana, nitafute nikupe bia 5,
 
Nina hakika wapo wabunge wengi waugwana ccm na wangeweza kupambana kama wao kurejea. Ile movie ya tamaa za kishindo imewakwaza wengi. Niwasihi nao pia waanzishe mapambana ndani ya Bunge kudai katiba bora.Ni aibu zama hizi kwa taifa letu kubwa kutegemea hisani ya Mtu badala ya mifumo imara. Tunafanya kufuru kumtukuza mwanadamu badala ya Muumba.
 
Chonde chonde Wabena na Wakinga, Jah People akionekana huko muwekeeni sumu tu afe tu. Huyu mbunge wenu hatutakii mema!!
 
Mpango wa CCM upo kwa hiyo huyo Mzee haoti bali ansema kilichomo ndani ya chama chake - Kwa hiyo tunakwenda kubadili na kuwa na mihula miwili miwili ya miaka saba saba, tunanza na Mzee tunamuongezea miaka 2 hadi 2027, hapo tunafanya uchaguzi Mzee ruhsa tena kugombea baada ya marekebisho ya katiba kwa hiyo tunampa tena 7 inafika 2034 afu anamalizia na muhula wa mwisho wa miaka 7 hadi 2041

Jumla atakuwa ametawala kwa miaka 5 + 5+ 2+ 7+ 7 = 26

Atamzidi Mwalimu kwa mwaka mmoja Mwalimu yeye aliyetawala miaka 25 - kwa hiyo kauli ya Mwalimu kwamba hakutakuwa na Rais atakayetawala muda mrefu kuliko yeye itakuwa imevunjwa rasmi na chama chake !! Asikudanganye mtu Urais ni mtamu aisee !!

CCM oyeeeeeeee
Bunge oyeeeeeeee
Maendeleo hayana vyama !!
 
Wamuongezee muda akatawale familia zao.Tumemchoka mno,tunangojea mi4 hii iishe asepe.

Watu waelevu na wazalendo tunaomba kila siku aondoke muda wake uishe haraka.


Kuna jamaa nimekaa naye hapa anasema anaomba hata akatize tu muda uliobaki kwa kuwa mateso yameshakuwa too much, namuambia asubirie tu dawa iishe asitake kukatiza DOZI.
 
Mafahali wawili wanapopigana Nyasi ndizo huumia, We know nothing about hao wakubwa kunyooshwa, kwa sababu baada ya kunyooshwa sijui anakula nini, anavaa nini, anaalala wapi.

Mengi tunasikia ni kuwa Fulani kahukumiwa kulipa Billion kadhaa. Then what next???
Mnyonge atajengewa nyumba kwa hizo billions of money? No. Atakuheshimu? Sidhani kwa sababu still hujui kabakiwa na nini

Ninachojua mimi sisi kama Watanzania wengi wetu hufurahi kuona mwingine akikandamizwa either kwa haki au kwa hila lakini we benefit nothing from it.

Huyo mtu anaefurahi kunyooshwa kwa wengine ili heshima iwepo utakuta hana nyumba since 2015 and I bet 2025 itamkuta hana nyumba lakin utakuta anafurahia mtu kama Manji kunyooshwa😬😬😬
 



Ama kweli yaliyomo YAMO!!
 
kuna mtanzania maskini sana aliambiwa achague tukupe milion 70 au tumtoe jicho lililobaki huyu jirani yako sababu yule jirani yake alikuwa chongo jicho moja!jamaa alijibu nyie mmalizie tu hilo jicho pesa sihitaji mimi.ndivyo watanzania tulivyo
 
Na hao tunaowaona kukosa nyuma wala wala mbele, wasiokua na nyumba wala mpango wa kuwa na nyumba ndio kundi kubwa ndani ya nchi.

Na hili kundi ndio walioondolewa kikwazo cha ada kwa watoto wao

Ndio waliopelekewa huduma za maji safi, barabara, shule, afya na umeme wa rea

Ndio wanaopiga simu kwenye kipindi cha Papokwapapo na Polepole na kutatuliwa kero zao

Ndio waliopewa relief na serikali pale wapendwa wao wanapoaga dunia wapewe miili wakazike hata kama wanadaiwa na hospitali

NA NDIO WAJUMBE NA WAPIGA KURA MAKINI KUCHAGUA KILE WANACHOKIAMINI

TUSIDHARAU MWIBA MGUU UKAOTA TENDE
 
kuna mtanzania maskini sana aliambiwa achague tukupe milion 70 au tumtoe jicho lililobaki huyu jirani yako sababu yule jirani yake alikuwa chongo jicho moja!jamaa alijibu nyie mmalizie tu hilo jicho pesa sihitaji mimi.ndivyo watanzania tulivyo
Wenyewe wanakuambia walikua wanajidai sana, sasa wacha tufanane

Kikubwa nilichojifunza hawa watu hawapendi kudharauliwa, ukiwaonyesha kuwaheshimu na kuwaelewa inatosha sanaaa. Lakini ukiwaita wajinga na maskini watakaa kimya na kukusubiri mkutane🤣🤣🤣🤣
 
Mtu haongelei maendeleo na changamoto za jimboni kwake , anaongea usengeh, anyway sisi tuko pembeni tunaendelea na shuhul zingine za kusaidia familia zetu, wao tuwaache wenyewe watakavyojiamulia mambo kwani nani atawauliza, waendelee kuwashwa nyuma na kujikuna vilevile wenyewe
 
Kuuliza kwamba mbunge aliwasiliana na waliomchagua kabla ya kuwasilisha hoja bungeni si sahihi. Nahisi unahoji hivyo kwa kuwa hoja husika hukubaliani nayo. Hoja ipi ambayo unakubaliana nayo ambayo mbunge aliita wananchi wa jimbo lake wakakubaliana kwamba awasilishe hoja hiyo?

Niseme wazi kwamba hata mimi sikubaliani kabisa na hoja ya kumwongezea muda Rais JPM kwani Bunge siyo chombo cha kumtungia sheria mtu mmoja mmoja kufuatana na jinsi anavyoonekana kwa mambo ya mpito bali kibaki chombo cha kutunga sheria za kudumu kwa manufaa ya nchi kwa ujumla. La sivyo itakuwa huyu aongezewe mitano; yule mitatu na mwingine ishirini, kufuatana na mihemko wanayoipata watu katika kipindi husika. Huu ni uchuro utakaoiharibu nchi.

Pamoja na kupinga hoja ya mbunge, tusitumie hoja za kuuliza kama mbunge ameshauriana na waliomchagua kabla ya kufikisha hoja bungeni. Hakuna mbunge anayofanya hivyo kama modus operandi. Uzuri ni kwamba JPM mwenyewe ameisha sema mara kadhaa kwamba hakubaliani na wazo hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…