Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
"Kwenye ziara za Viongozi na matamko ya Viongozi tumekuwa tukiambiwa barabara zitajengwa za Handeni - Kimirashi - Kiteto - Kondoa - Singida. Handeni - Tuliani - Morogoro lakini haikuwahi kutokea. Leo nasimama hapa kuthibitisha kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameleta mkandarasi kampuni ya China 🇨🇳 inafanya kazi usiku na mchana" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini"Leo inajengwa barabara ya lami kutoka Handeni - Kimirashi - Kiteto - Kondoa - Singida kilomita 434. Inajengwa barabara kutoka Magore - Tuliani - Mziha - Negelo - Kanata - Kwamagome - Kidereko - Handeni Mjini" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini
"Toka mwaka 1961 tangu tunapata Uhuru tumekuwa na Hospitali ya Wilaya ilihali siyo Hospitali ya Wilaya, zaidi ya miaka 50 imechakaa, watu wakienda kutibiwa wananyeshewa. Amekuja Rais Samia Suluhu Hassan ametoa Milioni 900 na anaendelea kutoa Milioni 900 kila mwaka kufanya ukarabati wa Hospitali na kujenga majengo mapya na Kazi Inaendelea sasa hivi" - Mhe. Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini
"Tumeshafumua mabati yote ya zamani, tumepiga mabati mapya. Mwaka huu tuna Milioni 900, sasa hivi tunaendelea na Jengo la Dharura (Emergency) la kisasa, tutajenga majengo mengine 21 kwa kadiri ambavyo Mheshimiwa Rais atazidi kutupatia fedha" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini
"Katika mazingira hayo, Rais wa namna hiyo anatokea mtu anambeza tu. Mbezeni Rais wetu lakini Wananchi wapo pamoja naye Rais Samia Suluhu Hassan" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini.