Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE ALOYCE KWEZI ATAKA AJIRA KWENYE MIRADI ZIZINGATIE VIJANA WA MAENEO YAO
Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mkoa wa Tabora, Mhe. Aloyce Andrew Kwezi akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2023-2024 ya Shilingi Trilioni 3.554 iliyosomwa na Waziri Mhe. Prof. Makame Mbarawa bungeni Jijini Dodoma Tarehe 22 Mei, 2023.
"Kaliua tumenufaika, kuna barabara inatokea Kaliua yaana Chagu Kazilambwa yenye KM 36. Rais Samia Suluhu Hassan ameleta Shilingi Bilioni 38 na barabara imefikia zaidi ya asilimia 90" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua
"Kwenye mkataba wa Reli, mradi wa SGR wa Tabora mpaka Kigoma unapitia Kaliua na ukarabati wa Reli ya Kaliua mpaka Mpanda unakwenda vizuri. Hii ni sababu ya kupongeza Serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais Samia Suluhu Hassan" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua
"Kwa sasa tunaendelea kufunga taa Kaliua Mjini kutoka Relini Kaliua mpaka Kasungu, Lami sehemu kubwa imekamilika chini ya Mkandarasi mzalendo Samota ambaye amejenga barabara ya Urambo kwenda Kaliua, wakandarasi hawa muwawezeshe na kama kuna madeni muwalipe kwa wakati" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua
"Kaliua, barabara ya mchepua ya Ushokola (Relini) mpaka njia panda ya kuunga Urambo zimebaki KM 2.3. Bajeti inayoanza mwezi Julai mmeweka KM 1, naomba ifikapo mwezi Julai ongezeni KM 1 ili zikamilike" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua
"Barabara ya Kiuchumi, Mpanda-Kaliua-Kahama, barabara hii imewekwa kwenye Ilani ya CCM zaidi ya Mara tatu. Mimi ni muumini wa utekelezaji, kwenye bajeti ya Katavi mmeweka ujenzi wa daraja, ninaomba daraja hilo lianze mara moja, lisiishie kwenye kuandika bila utekelezaji" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua
"Naungana na Mbunge wa Katavi, tuko pamoja tunategemea mazao ya Tumbaku kutoka Mpanda kuja Kaliua kwenda Tabora na safari zingine yawe safari nzuri. Mazao ya Asali tunayategemea sana, Mahindi na Mchele. Ninaomba barabara ikamilike kwa wakati" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua
"Barabara ya kwenda Kigoma KM 36 mchepuo wa kwenda Ugansa-Usinge ndiyo kilio kikubwa cha WanaKaliua. Mradi upo chini ya mfadhili OPEC. Fedha ipo, kwanini msianze hizo KM 7? Wazee wa Usinge kila siku wanapiga simu, Mzee George Kamsimi, Juma Kitakala, Malabe, Madebo, Kakobe, Mama Mau na Rehema Hamis" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua
"Kwenye suala la Reli ya SGR Kaliua ni njiapanda, hizi ajira zinapojitokeza hakikisheni wenyeji wamepata ajira hizi, Vijana wa Kaliua, Mpanda na Kigoma wapo wa kutosha, wasihame na watu kutoka mbali. Fuatilieni ukarabati wa Kaliua-Mpanda unahitaji wenyeji wapate. Zipo kazi ambazo hazihitaji Shule ila zinahitaji nguvu, si mnasemaga mzigo mzito muwape Wanyamwezi sasa mnakwepaje mnahama na watu!" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua
"Jambo kubwa kwenye Reli, ninaomba kuna vituo kabla ya stesheni na stesheni katikati wanatozwa faini wanakijiji wanapovuka kutoka Kijiji A kwenda Kijiji B, naomba Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ufuatilie jambo hilo" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua