Mbunge Livingstone Lusinde amtaka Spika Ndugai ajiuzulu, asema hata ombi lake la msamaha lilikuwa la uongo

Mbunge Livingstone Lusinde amtaka Spika Ndugai ajiuzulu, asema hata ombi lake la msamaha lilikuwa la uongo

Mbunge wa jimbo la Mtera Livingstone Lusinde amemtaka Spika Job Ndugai ajiuzulu kufuatia kauli aliyoitoa kupinga serikali kuchukua mikopo. Lusinde amesema alianagalia clip yote ya mazungumzo ya Job Ndugai na hakuna sehemu iliyounganishwa ili kumchonganisha na Rais kama yeye (Ndugai) alivyosema, alieleza zaidi kuwa hayo yalikuwa ni maneno yake na hivyo hata katika uombaji wake wa msamaha hakuwa na sababu ya kukanusha alichokisema. Lusinde amemtaka Spika Ndugai kujiuzulu mara moja ili kuwatendea haki wagogo pamoja na wakazi wa mkoa wa Dodoma ambao ni wanufaika mkubwa wa mkopo uliochukuliwa na serikali.
View attachment 2070646
Ukiona Lusinde,Gwajima na Msukuma hawako upande wako wala hawakutetei basi jifungashe mapeeeema,maana hawa ndio wapuuzi wenyewe aliowasema Ustadh Kundecha.
 
Mbunge wa jimbo la Mtera Livingstone Lusinde amemtaka Spika Job Ndugai ajiuzulu kufuatia kauli aliyoitoa kupinga serikali kuchukua mikopo. Lusinde amesema alianagalia clip yote ya mazungumzo ya Job Ndugai na hakuna sehemu iliyounganishwa ili kumchonganisha na Rais kama yeye (Ndugai) alivyosema, alieleza zaidi kuwa hayo yalikuwa ni maneno yake na hivyo hata katika uombaji wake wa msamaha hakuwa na sababu ya kukanusha alichokisema. Lusinde amemtaka Spika Ndugai kujiuzulu mara moja ili kuwatendea haki wagogo pamoja na wakazi wa mkoa wa Dodoma ambao ni wanufaika mkubwa wa mkopo uliochukuliwa na serikali.
View attachment 2070646
Huyu asingemsagia kunguni ndugai ningeshangaa sana maana hata kile kikao cha wagogo walialikwa wagogo wenye degree tu,sasa lusinde asimsindikize ndugai kwanini?
 
Naona uspika unanukia kwako; endelea kupalilia ila Tulia!
 
Mama atangaze haraka baraza la mawaziri kunusuru baadhi ya heshima za baadhi ya watu.

Funzo moja, ukiwa kwenye madaraka, tenda haki na fuata sheria, usikandamize watu.
 
Ndugai kawa kama Sabaya na Makonda ni watoto YATIMA ambao walipendwa sana na baba yao sasa wameachwa kwa mama wa kambo mwenye watoto wake.

acha tugonge mtori nyama tutakutana nazo chini
 
Ndugai kawa kama Sabaya na Makonda ni watoto YATIMA ambao walipendwa sana na baba yao sasa wameachwa kwa mama wa kambo mwenye watoto wake.

acha tugonge mtori nyama tutakutana nazo chini
Mlifurahi alichomfanyia Tundu Lisu?

KARMA malipo ni hapahapa duniani.
 
Hivi mmesikiliza Mzèe Jaji mstaafu Warioba? Tuwe wamoja kukabiliana na matatizo yanyotukumba.
 
Kifo Cha Magufuli kimeonyesha wap panavuja

Mama usizibe matundu nunua bati mpya hata kwa kukopa sawa tu

Hii inaitwa FROM HERO TO ZERO

Kamanda SIRO hii ni alarm kwako

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Malipo ni hapa hapa duniani. Mungu wetu ni kijana mnoo.. Kuna alie ua watu sasa nae kesha oza. Ndugai akiona uspika kama Mungu wa mjengoni. Leo ana sulubiwa, Lissu ana kula bata. Yaani, Ccm mtafika motoni mkiwa mmechoka sana.

wewe ni mpumbavu sana mkuu,sijui kama familia yako imetaarifiwa.
 
Lissu alishasemaga,wanaccm msifurahie kuteswa na kuumizwa sie wapinzani,wakishatumaliza sie watakuja kwenu,ndicho ninachokiona
 
Mgogo sawa na mmakonde. Msaidie chochote kesho hata sura yako haikumbuki.
Nimekua Dodoma vile vile nimekaa Mtwara na mikoa mingine mingi.
Shy , Toronto, that etc
Hahahaaaaa![emoji23][emoji23][emoji117] wanakuona na wanakusikia
 
Back
Top Bottom