Mbunge Luhaga Mpina ndoto yako ya kuwa mbunge maarufu Tanzania imetimia

Mbunge Luhaga Mpina ndoto yako ya kuwa mbunge maarufu Tanzania imetimia

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Leo hii ukiulizwa mbunge maarufu Tanzania kwa kujenga hoja zenye mantiki hutakosa kumtaja mbunge Mpina.

Amezichanga karata vizuri akatumia nafasi yake vizuri katika kipindi hichi wala hakuchagua kuketi upande wa walamba asali.

Ameamua kusimama pamoja na wananchi wa Tanzania. Amezibeba kero; na mioyo ya watanzania. Ndio maana hakosi vitu vya kuongea hakosi point za kuongea akiwa bungeni.

Hongera kwa kuzisoma nyakati. Enzi zile tulikua na wakina Tundu Lissu leo hii tuna wakina Luhaga Mpina.

Mawasiliano: menejawamakampuni@gmail.com
 
Hahahhaha wabunge wa hivyo CCM wapo wengi sana wote ni kufukuzia uwaziri tu. Bashe alikua anapambania wananchi sio kidogo bunge vipi baada ya uwaziri? Mwita Waitara wa kabla ya uwaziri na baada ya unaibu waziri wanafanana?

Hao CCM ni wachumia tumbo hakuna ambaye yupo serious. Kina Kabudi, Bashiru, na Polepole wawe funzo kwetu. Walipigania katiba ila walipopata umaarufu Hadi kupewa vitengo wakakana umuhimu wa katiba mpya!!

So tusubiri Tena Mpina apate unaibu waziri akane hizi kauli zake then turudi hapa kulialia kuwa kateguka.
 
Hahahhaha wabunge wa hivyo CCM wapo wengi sana wote ni kufukuzia uwaziri tu. Bashe alikua anapambania wananchi sio kidogo bunge vipi baada ya uwaziri? Mwita Waitara wa kabla ya uwaziri na baada ya unaibu waziri wanafanana...
Mpina alikua Waziri... Lkn alihakikisha anawadhibiti wavuvi haramu kwelikweli

Unajua uongozi wa Damuni, haunaga mbambamba..
 
Hahahhaha wabunge wa hivyo CCM wapo wengi sana wote ni kufukuzia uwaziri tu. Bashe alikua anapambania wananchi sio kidogo bunge vipi baada ya uwaziri? Mwita Waitara wa kabla ya uwaziri na baada ya unaibu waziri wanafanana...
So, baada ya kukusoma nimepata swali kwako, je, tuzipuuze hoja zake anazotoa sasa kisa mbele atatugeuka kama akiupata uwaziri? au tumsikilize?

Kama unataka tumpuuze, tuoneshe nani mwingine atakayeziba pengo la Mpina kuwa bubu kule bungeni, hasa ukizingatia hakuna wapinzani wanaoeleweka waliopo bungeni kwa sasa..
 
Hahahhaha wabunge wa hivyo CCM wapo wengi sana wote ni kufukuzia uwaziri tu. Bashe alikua anapambania wananchi sio kidogo bunge vipi baada ya uwaziri? Mwita Waitara wa kabla ya uwaziri na baada ya unaibu waziri wanafanana...
Mpina hajaanza leo hii haiba ila Magufuli tuu ndie alimpoteza kwenye uwaziri
 
Kwa bunge kibogoyo ni kama anafurahisha genge. Alishiriki muda wote kuona nguvu na heshima ya bunge inapunguzwa kisa aliona wapinzani wanapata uungwaji mkono.

Kwasasa anapiga kelele lakini tayari serikali na wananchi wamelipuuza bunge.
 
Hahahhaha wabunge wa hivyo CCM wapo wengi sana wote ni kufukuzia uwaziri tu. Bashe alikua anapambania wananchi sio kidogo bunge vipi baada ya uwaziri? Mwita Waitara wa kabla ya uwaziri na baada ya unaibu waziri wanafanana...
Uko sahihi kabisa, kumshabikia mtu ambaye misimamo yake inabadilika kutokana na ulaji ni kupoteza Muda. Kibaya zaidi hilo bunge kwa sasa halina meno.
 
Vipi na wewe ile ndoto yako ya kuwa Mbunge ktk moja ya majimbo kule Songwe bado ipo? Jimbo la Mbozi Mashatiki😂😂
Nenda Polepole, mwenzio Lucas mwashambo anakufuatilia kwa karibu sana.
2025 napeperusha bendera sio utani. Nahitaji kufanya mabadiriko katika jimbo la Mbozi.
 
Mpina Magufuli ajaye ila mfumo ushamkataa chama hakiwezi kurudia kosa labda Mkapa angekuwepo 2030 patachimbika hao watu wa kanda ya ziwa
 
2025 napeperusha bendera sio utani. Nahitaji kufanya mabadiriko katika jimbo la Mbozi.
Hebu yalist hapa tuone kama mambo mapya kabisa😂😂

Kama Spika wa Bunge pamoja na kuwa Mkuu wa mhimili anashindwa kufanya mabadiliko yoyote jimboni kwake wewe utakuja Na mwarobaini gani?

Labda utajifanyia mabadiliko kwa kuanza kula kodi ya wananchi aka kulamba asali.
 
Leo hii ukiulizwa mbunge maarufu Tanzania kwa kujenga hoja zenye mantiki hutakosa kumtaja mbunge Mpina...
Naunga mkono hoja, na kwa geopolitics za nchi yetu, mmoja kati ya wawili hawa, VP na PM wa 2025 lazima atoke Kanda ya Ziwa!, huu sio ubaguzi na wala sio mimi, hii ni geopolitics ya siasa za nchi yetu.

Hivyo Kanda ya Ziwa katika umoja wetu, tunampendekeza Luhanga Mpina kuendelea kugombea ubunge kupitia CCM, ili awe Waziri Mkuu wa 2025 na CCM wakifanya kosa la kumuengua, atasimama na upinzani na anashinda, sasa mtu kama huyu akiirejea Bungeni kupitia upinzani, ukizingatia Mbowe anarejeshewa Hai yake, Lissu lili lile jimbo lake, Zitto anarejea kupitia Kigoma, sipati picha ya hilo Bunge la 2025 - 2030!.
P
 
Back
Top Bottom