Mbunge Luhaga Mpina ndoto yako ya kuwa mbunge maarufu Tanzania imetimia

Mbunge Luhaga Mpina ndoto yako ya kuwa mbunge maarufu Tanzania imetimia

Leo hii ukiulizwa mbunge maarufu Tanzania kwa kujenga hoja zenye mantiki hutakosa kumtaja mbunge Mpina.

Amezichanga karata vizuri akatumia nafasi yake vizuri katika kipindi hichi wala hakuchagua kuketi upande wa walamba asali.

Ameamua kusimama pamoja na wananchi wa Tanzania. Amezibeba kero; na mioyo ya watanzania. Ndio maana hakosi vitu vya kuongea hakosi point za kuongea akiwa bungeni.

Hongera kwa kuzisoma nyakati. Enzi zile tulikua na wakina Tundu Lissu leo hii tuna wakina Luhaga Mpina.
Alikuwepo Lucas Selelii, Sasa hivi Yuko kalala kwenye makaburi ya kisiasa, na alikuwa na hoja kweli, acha huyo masulupwete
 
So, baada ya kukusoma nimepata swali kwako, je, tuzipuuze hoja zake anazotoa sasa kisa mbele atatugeuka kama akiupata uwaziri? au tumsikilize?

Kama unataka tumpuuze, tuoneshe nani mwingine atakayeziba pengo la Mpina kuwa bubu kule bungeni, hasa ukizingatia hakuna wapinzani wanaoeleweka waliopo bungeni kwa sasa..
Nani ataziba pengo? HAYUPO maana CCM ndio Ina wabunge 95% na wote hao wako pale sababu ya kulinda maslahi ya serikali. Ni kheri tutegemee hata wanaharakati, waandishi wa habari kupaza sauti kwenye matatizo yetu ila sio mbunge wa CCM wanatuchora tu wale maana wametugeuka sana Kila tulipowaamini.
 
Naunga mkono hoja, na kwa geopolitics za nchi yetu, mmoja kati ya wawili hawa, VP na PM wa 2025 lazima atoke Kanda ya Ziwa!, huu sio ubaguzi na wala sio mimi, hii ni geopolitics ya siasa za nchi yetu. Hivyo Kanda ya Ziwa katika umoja wetu, tunampendekeza Luhanga Mpina kuendelea kugombea ubunge kupitia CCM, ili awe Waziri Mkuu wa 2025 na CCM wakifanya kosa la kumuengua, atasimama na upinzani na anashinda, sasa mtu kama huyu akiirejea Bungeni kupitia upinzani, ukizingatia Mbowe anarejeshewa Hai yake, Lissu lili lile jimbo lake, Zitto anarejea kupitia Kigoma, sipati picha ya hilo Bunge la 2025 - 2030!.
P
Hamna kitu, mbona Mpina wamemkata ujumbe wa NEC mkoa na kitaifa ila hakuna madhara yoyote? Hamna kitu atafanya hata aligombea upinzani wataiba kura na maisha yataendelea. Kwa katiba hii hakuna wa kumchallenge mwenyekiti wa CCM
 
Leo hii ukiulizwa mbunge maarufu Tanzania kwa kujenga hoja zenye mantiki hutakosa kumtaja mbunge Mpina.

Amezichanga karata vizuri akatumia nafasi yake vizuri katika kipindi hichi wala hakuchagua kuketi upande wa walamba asal...
Huyu angekuwa mbunge wa kuteuliwa leo hii tungesikia kapewa ubalozi Zimbabwe.
 
Leo hii ukiulizwa mbunge maarufu Tanzania kwa kujenga hoja zenye mantiki hutakosa kumtaja mbunge Mpina.

Amezichanga karata vizuri akatumia nafasi yake vizuri katika kipindi hichi wala hakuchagua kuketi upande wa walamba asali.

Ameamua kusimama pamoja na wananchi wa Tanzania. Amezibeba kero; na mioyo ya watanzania. Ndio maana hakosi vitu vya kuongea hakosi point za kuongea akiwa bungeni.

Hongera kwa kuzisoma nyakati. Enzi zile tulikua na wakina Tundu Lissu leo hii tuna wakina Luhaga Mpina.

Alipogusia katiba mpya nikamuona wa maana. Namuunga mkono kwenye Hilo.
 
Hamna kitu, mbona Mpina wamemkata ujumbe wa NEC mkoa na kitaifa ila hakuna madhara yoyote?
Kwa sasa yes it's true Mpina hana madhara, lakini 2025, it's not!.
Hamna kitu atafanya hata aligombea upinzani wataiba kura na maisha yataendelea.
Kuna vitu kiongozi mwanaume anaweza kufanya lakini Mwanamke hawezi, Mwanamke hawezi kuwa mwizi!, ni aibu!.
Kwa katiba hii hakuna wa kumchallenge mwenyekiti wa CCM
It's true na sio tuu kumchallenge Mwenyekiti bali Tanzania hatuna upinzani wa kui challenge CCM!.
P
 
Hebu yalist hapa tuone kama mambo mapya kabisa😂😂

Kama Spika wa Bunge pamoja na kuwa Mkuu wa mhimili anashindwa kufanya mabadiliko yoyote jimboni kwake wewe utakuja Na mwarobaini gani?

Labda utajifanyia mabadiliko kwa kuanza kula kodi ya wananchi aka kulamba asali.
Kazi kwako mheshimiwa wa Mbozi, jimbo linataka kukuponyoka hilo
 
Back
Top Bottom