Tetesi: Mbunge machachari kutikisa siasa za Tanzania na kumwaga manyanga kabla ya Julai 24

Tetesi: Mbunge machachari kutikisa siasa za Tanzania na kumwaga manyanga kabla ya Julai 24

Status
Not open for further replies.
Maccm mnapataga faida gani kuuharibu upinzani?? Kueni jamani. Nchi bila upinzani haiongozekiiiiiiii. Ah! Yaani mna maudhi mpaka baasi tena.
Aseme atakalo. Aondoke kesho asubuhi. Tume ya uchaguzi ipime, muda ukifika turudi chunguni apikwe mwingine. Shida yenu ni kuona hakuna upinzani tena Tz au nini?? Mbona bunge mlibaki peke yenu, mliongeza nini au mlipunguza nini??
Tulikuwa na kina Tuntemeke Sanga kwenye bunge la chama kimoja, wapinzani kweli kweli. Wakashika shilingi, bajeti ikatikisika. Wako wapi, Leo si bado tupo?
Msiogope, hakuna njia kuwa upinzani utakufa. No, ukiondoka huu utaanza mwingine, hata ccm kwa ccm.
 
Aondoe fukuto ndani ya moyo wake. Kama ni kweli, atakuwa wa kwanza kuonyesha madhara ya kubadili gia angani.
 
Wasalaam wana jamvi!

Niendelee kuwatakia sikukuu njema ya amani na furaha miongoni mwenu!

Wana jamvi kama mtakumbuka siasa za tanzania zilitikiswa mwaka jana kama mara tatu hivi
Mara ya kwanza ilikuwa ni mtuhumiwa wa ufisadi kuhami upande mwingine..wengi hawakutegemea kama atapokelewa.

Mara ya pili ilikuwa kwa nguli wa siasa na Mzalendo Dr Slaa kumwaga manyanga chanzo ikiwa ni kupinga ujio wa mtuhumiwa wa ufisadi kwenye chama chao na hakuwa tayari kushiriki dhambi ya kumsafisha!

Tatu ilikuwa ni pale Prof Msomi na nguli wa uchumi alipo kataa kushiriki dhambi ya kumsafisha mtuhumiwa wa ufisadi na kuamua kumwaga manyanga!

Sasa kabla ya tarehe 24 nchi itatekwa tena na taharuki ya aina yake baada ya mbunge kijana na machachari kuvunja ukimya na kuamua kumwaga manyanga!
Taarifa zinasema mbunge huyo amekuwa kimya kwa kipindi kirefu sana na amekuwa akizushiwa anaumwa ili ionekane hiyo ni sababu kuu!

Hata hivyo amekuwa akipata wakati mgumu sana hasa pale anapo lazimishwa kutoa matamko ili ionekane yupo pamoja nao na amekuwa akikataa na kusema sitaki kuongea na kusema fulani aongee..

Jambo hili limekuwa likiwatesa sana watu wake ndani ya umoja wao na chama chao kwani ukimya wake umekuwa ukizua maswali mengi na wamejaribu kila mbinu za kumlazimisha aongee lakini wameshindwa!

Jambo la kumlazimisha aongee limekuwa likimkera sana na amekuwa akiwa sisitiza kuwa yeye amechagua kunyamaza wasi mlazimishe!

Kibaya zaidi kuna mpango wa kumlazimisha kuongea kwenye mkutano fulani tarehe 24 ambao bado haujawa confirmed! Lakini baada ya kupata habari kuwa amepangwa kuongea na kusema hataki na wasimlazimishe kwani umoja una watu wengi wa kuongea!

Sasa habari zilizopo ana mpango wa kuongea na ataongea kinacho muumiza kabla ya tarehe 24 na atamwaga manyanga na kuachana na ubunge kabisa na kwenda kusoma nje ya nchi....

Baada ya viongozi wake kupata habari hizo wanahaha kumzuia asiongee huku wakitaka kujua anataka kuongea nini na wanampango wa kuhakikisha aengei chochote na wameshambembeleza sana lakini amesimama kuwa kwenye msimamo wako kuwa ataongea kabla ya tarehe 24!

Zina fanyika kila juhudi za kunusuru tukio hilo kwani wanasema litasambaratisha umoja huo kabisa.

Lakini amesisitiza kuwa hayuko tayari kushiriki siasa za kinafiki kamwe...!

Je watafanikiwa kumzuia?
Ni nani huyo?
Ataendelea kukaa kimya?
Ni kwañini hawataki aongee?

Wana jamvi muda huongea tusubiri!

Karibuni wana jamvi!
Well said
 
Siiamini sana hii taarifa japo ina harufu ya ukweli ndani yake.
Nnachotafakari tu why hakujitenga mara tu baada ya kutambua uozo umeingia? Kwanini awapotezee muda wapigakura wake na kuliingiza hasara taifa kwa mchakato mwingine wa uchaguzi mdogo?
Bado ntaendelea kumuona mnafiki ni mara mia akaachana na uamzi huo na kujikita kuwatumikia wanajimbo make ndo jukumu kuu walilomtuma akawakilishe.
 
Soma hiki kibonzo.
Msitu wenye nyasi za wastani unaitwa NYIKA.
Na kama mtu niwakabila fulani utasema:
Mchaga
Mmachame
Mnyiramba.
Je anaetoka kwenye kabila la WANYIKA angeitwaje?
Je umeshamjua mbunge mwenyewe?
 
Watanganyika waajabu sana. Hivi kuna kitu gani cha ajabu mtu akiachia nafasi alionayo? Hivi ninani mkubwa kuliko nguvu ya Watanganyika? Wangapi wakubwa zaidy ya hizi dagaa wamepita na hakuna anguko lolote? nchi bado inasonga

Kwa kweli, kama ni JJ aende tu, na angekuwa na busara angekaa kimya na kuachana na siasa tena mwaka 2020..walah sio mbali! Kubwa katika hili ni kuwa, alichaguliwa na kuna watu wanaimani naye, sio kweli kwamba watateseka sana.

NYERERE alitufaa sana, ameondoka, Sokoine tulishangilia sana, ameondoka. wakaja wanganga wakaganga wametoka, kwa sasa hata upinzani, mecho yote kwa Mzee Pombe. JJ ni nani?

Kama ni Umbea wa Kwenye Sosho Media Ubaki Kuwa Umbea ...Lkn Kama JJ ana Akili Hizi Akae Mbali..

Huu Ndio Mchango Wangu
 
Ubunge aliomba mwenyewe alipita kwenye kura za maoni akashinda akakesha usiku kuchaa kulinda kuraa akashindaa akatangazwaa akasherehekea! Sasa hata kam! akimwaga manyanga hiyo pia itakua ni maamuzi yake haitatikisa kitu sbbu yeye ndo aliomba kura kwa wananchi so akiamua kuachia ngazi ni yeye sioni nchi kutikisika!
Kumbuka uchaguzi wa ndani ya chama ktk jimbo aliloshinda uliahilishwa mala mbili baada ya kutokutokea, mala ya tatu ndiyo akaja kinyonge hata kampeni asisingizia anaumwa
 
Kuwe na criteria za kuanzisha uzi sio mtu yupo chooni anaanzisha uzi mnapoteza credibility ya jf
 
Wasalaam wana jamvi!

Niendelee kuwatakia sikukuu njema ya amani na furaha miongoni mwenu!

Wana jamvi kama mtakumbuka siasa za tanzania zilitikiswa mwaka jana kama mara tatu hivi
Mara ya kwanza ilikuwa ni mtuhumiwa wa ufisadi kuhami upande mwingine..wengi hawakutegemea kama atapokelewa.

Mara ya pili ilikuwa kwa nguli wa siasa na Mzalendo Dr Slaa kumwaga manyanga chanzo ikiwa ni kupinga ujio wa mtuhumiwa wa ufisadi kwenye chama chao na hakuwa tayari kushiriki dhambi ya kumsafisha!

Tatu ilikuwa ni pale Prof Msomi na nguli wa uchumi alipo kataa kushiriki dhambi ya kumsafisha mtuhumiwa wa ufisadi na kuamua kumwaga manyanga!

Sasa kabla ya tarehe 24 nchi itatekwa tena na taharuki ya aina yake baada ya mbunge kijana na machachari kuvunja ukimya na kuamua kumwaga manyanga!
Taarifa zinasema mbunge huyo amekuwa kimya kwa kipindi kirefu sana na amekuwa akizushiwa anaumwa ili ionekane hiyo ni sababu kuu!

Hata hivyo amekuwa akipata wakati mgumu sana hasa pale anapo lazimishwa kutoa matamko ili ionekane yupo pamoja nao na amekuwa akikataa na kusema sitaki kuongea na kusema fulani aongee..

Jambo hili limekuwa likiwatesa sana watu wake ndani ya umoja wao na chama chao kwani ukimya wake umekuwa ukizua maswali mengi na wamejaribu kila mbinu za kumlazimisha aongee lakini wameshindwa!

Jambo la kumlazimisha aongee limekuwa likimkera sana na amekuwa akiwa sisitiza kuwa yeye amechagua kunyamaza wasi mlazimishe!

Kibaya zaidi kuna mpango wa kumlazimisha kuongea kwenye mkutano fulani tarehe 24 ambao bado haujawa confirmed! Lakini baada ya kupata habari kuwa amepangwa kuongea na kusema hataki na wasimlazimishe kwani umoja una watu wengi wa kuongea!

Sasa habari zilizopo ana mpango wa kuongea na ataongea kinacho muumiza kabla ya tarehe 24 na atamwaga manyanga na kuachana na ubunge kabisa na kwenda kusoma nje ya nchi....

Baada ya viongozi wake kupata habari hizo wanahaha kumzuia asiongee huku wakitaka kujua anataka kuongea nini na wanampango wa kuhakikisha aengei chochote na wameshambembeleza sana lakini amesimama kuwa kwenye msimamo wako kuwa ataongea kabla ya tarehe 24!

Zina fanyika kila juhudi za kunusuru tukio hilo kwani wanasema litasambaratisha umoja huo kabisa.

Lakini amesisitiza kuwa hayuko tayari kushiriki siasa za kinafiki kamwe...!

Je watafanikiwa kumzuia?
Ni nani huyo?
Ataendelea kukaa kimya?
Ni kwañini hawataki aongee?

Wana jamvi muda huongea tusubiri!

Karibuni wana jamvi!
Mbona ameshaongea aliomba kwa ridhaa yake na anaachia kwa ridhaaa yake kipi kipya?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom