Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mbunge wa Sumve (CCM), Kasalali Mageni, ameelezea wasiwasi wake kuhusu mchakato wa ajira serikalini unaotegemea ‘connection’, akidai kuwa mfumo huu unazalisha watumishi wasiokuwa na sifa zinazostahiki, hivyo kusababisha hasara kwa serikali.
"Wengi wanaamini ajira bila connection haipatikani, ndio maana sisi Mbunge ni mashahidi, kila Mbunge kwenye Jimbo lake ana meseji lukuki za kuombwa kusaidia watu wapate ajira"
"Kwahiyo Watu wanaoajiriwa kwa kuamini connection ndio imewapa ajira wanapoingia ofisini wanaenda kufanya kwa connection hizo hizo, kwahiyo mwisho wa siku tunapata hasara ya pesa zetu. "
Ameongeza kuwa ipo haja ya kuangalia mifumo inayotumika kuwapata Wakuu wa Mashirika ya Umma, Wakurugezi kwenye Halmashauri na namna wavyopatikana Makatibu Tawala.
"Ifike mahali tujiulize, tunahitaji Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kazi gani?, anahitajika mtu mwenye sifa zipi akawe mkurugenzi wa Halmashauri? Au tunaweka mtu tu akajaze nafasi, tujifunze kutoka kwa mabenki, nafasi ya kazi inatangazwa ndani ya wafanyakazi wenye sifa"
Soma: Mbunge Shabiby: Wapigaji wameongezeka serikalini, sitasifia kila kitu