Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungumza wakati wa mjadala Bungeni kuhusu Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyowasilishwa Bungeni Mwaka wa Fedha 2022/23, leo Oktoba 31, 2024, Mbunge wa Sumve, Kasalali Mageni amesema imekuwa kawaida kuona Ripoti hiyo kuwa na mambo yaleyale ya wizi na uzembe hali inayoonesha kuna shida kuanzia kwenye mfumo wa Uajiri wa Watumishi wa Umma.
Amesema hali ilivyo sasa ni kuwa wengi wanaamini kuwa na “connection” huwezi kupata ajira Serikalini na Watu hao wanapopata ajira hata utendaji wao hazingatii misingi ya ajira zao.