Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHANDISI MAGESA AKEMEA UPOTOSHAJI MRADI WA MAJI CHANKOLONGO
Mbunge wa Jimbo la Busanda, Mhandisi Tumaini Magesa amewatoa hofu wananchi wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro juu ya mradi wao wa maji wa Chamkolongo unaondelea kutelekelezwa kwani umefikia hatua za mwisho kumalizika na kupuuza maneno ya watu yalioenezwa kuwa mradi ulianzishwa kukidhi mbio za mwenge peke yake.
Magesa amesema hayo wakati akikabidhi kompyuta mpakato kwa viongozi pamoja na wafanyabiashara wa Katoro ambayo ni moja ya ahadi yake ya mwaka 2021 baada ya kuingia madarakani.
Amesema walichokifanya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Geita (GEUWASA) ni sahihi kitalaamu na kwa mjibu wa mkataba na wala mradi na si kwa ajili ya mbio za mwenge.
"Rais ameendelea kuleta fedha kwenye mradi huu lengo ni kuwa Katoro pawe na maji ya uhakika na salama" Amesema Mhandisi Magesa.