Mbunge Maimuna: Barabara ya Kibiti-Lindi ina viraka milioni 10 kabla haijakabidhiwa

Mbunge Maimuna: Barabara ya Kibiti-Lindi ina viraka milioni 10 kabla haijakabidhiwa

Hiyo barabara aliikataa magufuli lakini mkandarasi akaongea na fisadi namba Moja(rais wa wakati ule).ikabidi alikubali tu Kwa shingo upande.
Barabara ilijengwa na kampuni ya china CHICCO nadhani,ambao walijenga kipande Cha manyoni-dom,jakaya alimrithi huyo mkandarasi,nakumbuka Waziri mramba alilalama bungeni kuwa mkandarasi mjeuri, mkandarasi alidai Hana pa kupata changarawe/kokoto za kujengea barabara
 
Babara kutoka Mkuranga mpaka Mtwara na kutoka Mnazi mmoja mpaka Mangaka inapaswa kufumuliwa ijengwe tena.
Kipande cha barabara kutoka Tunduru, Namtumbo mpaka Songea kilichojengwa kwa ufadhili wa "Millennium Challenge"ya Marekani kiko poa sana
 
Barabara ya kuanzia Dar kwenda mtwara inahitaji marekebisho/matengenezo

Kiufupi Barabara huko kusini maeneo mengi yanahitaji matengenezo tu
Kwa sasa hivi unapotoka dar es salaam kwenda karibia mikoa yote barabara zimejaa viraka balaa..mpaka city centre ni viraka, mashimo na madimbwi.Hii ni aibu kubwa...
 
Back
Top Bottom