Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Hili limetokea baada ya Wakili Mwabukusi kutoa kauli mbalimbali kuhusu bandari ikiwemo kusema Watanzania wasimuamini Waziri Mkuuu kwani ni muongo, na kwenda kufungua kesi ya kuishtaki Serikali ya Tanzania kuingia Mkataba wa Bandari na kampuni wa DP World.
Mariam amesema Wakili Mwabukusi amekuwa anatumia lugha ambazo sio za kiungwana, zilizojaa kebehi dharau, zilizovuka mipaka, ubaguzi na kichochozi, pamoja na kutweza utu viongozi mbalimbali ikiwezo Rais Samia, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, pamoja na wananchi.
Mariam ameongeza kuwa baadhi ya kauli za Wakili Mwabukusi zinaaibisha taaluma yake kwani zinavunja sheria za nchi yetu. Akisema, wakili anajua fika akishafungua shauri Mahakamani hatakiwi kutoa maoni ili Mahakama itoe maamuzi kwa uhuru na haki, lakini pia kavunja Sheria ya Makosa ya Kimtandao kwa kutukana na kutumia lugha za kibaguzi.
Mariam Ditopile amesema kauli za Wakili Mwabukusi asipokemewa anaweza kuleta taharuki, uvunjifu wa amani au machafuko katika nchi yetu.
Pia soma
Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika
Mawakili wa Wananchi waomba Shughuli zote za DP World kwenye bandari za Tanzania zisitishwe hadi kesi itakapomalizika
Adv Mwambukusi: Watanzania bora mumwamini shetani na siyo Waziri Mkuu