Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge Martha Mariki Achangia Zaidi ya Milioni 6 UWT kusaidia Ujenzi wa Nyumba za Watumishi
MBUNGE wa Viti maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki anechangia mifuko 30 ya Simenti na fedha shilingi milioni Moja kwaajili ya kusaidia ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi wa UWT Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.
Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki anechangia mifuko 30 ya Simenti na fedha shilingi milioni Moja kwaajili ya kusaidia ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi wa UWT Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Akikabidhi simenti hiyo kwa mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mlele kwa niaba ya Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki,Katibu wa Mbunge huyo Teddy Ndasi amesema kuwa Mbunge martha mariki amemtuma kuja kuwasilisha fedha na mifuko 30 ya Simenti.
‘’Kwa niaba ya Mh Martha amenituma kujakukabidhi mifuko hii 30 ya Simenti Pamoja na shilingi Milioni moja kwaajili ya kusaidia ujenzi wa Nyumba ya mtumishi wa UWT Wilaya ya mlele kwa niaba yake naomba kuwasilisha kwa mwenyekiti wa UWT Wilaya ya mlele amesema'' - Katibu huyo Teddy Ndasi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mlele Azama Mbogo amemshukuru Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki kwa Kuguswa na kuchangia mifuko 30 ya Simenti Pamoja na Shilingi Milioni moja kwaajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa UWT Wilaya ya Mlele.
"Nichukue nafasi hii kumushukuru sana Mbunge Martha kwa Msaada huu tumeupokea na tunaimani utatusaidia sana kuendeleza ujenzi wetu wa nyumba ya mtumishi wa UWT Wilaya ya Mlele tunamwahidi tutakwenda kuufanyia kazi msaada huu kwa malengo yaliyokusudiwa" - amesema Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mlele Azama Mbogo wakati wa Makabidhiano hayo
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amewaomba wanachama wa UWT kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano kwenye jumuiya ya UWT
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mlele Joshua Mbwana amemshukuru mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi kwa kuendelea kukisaidia chama cha mapinduzi Wilaya ya Mlele na UWT kwa ujumla.
"Tunamshukuru sana mbunge martha mwezi wa nane alitupatia chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mlele Mifuko 50 ya Simenti kwaajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya chama na leo tumepokea mifuko 30 ya simenti na shilingi milioni moja ameonyesha upendo wa dhati kwa chama chetu na UWT" - amesema Joshua.
Ikumbukwe kuwa Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi martha mariki kwa nyakat tofauti ameweza kutoa mifuko 30 ya Simenti na Shilingi Milioni Moja kwa UWT Wilaya ya Mpanda, Wilaya Tanganyika,na UWT Mkoa na leo ametoa ametoa mifuko 30 ya Simenti na Shilingi milioni moja ili kusaidia ujenzi wa Nyumba ya mtumishi wa UWT Wlaya ya Mlele.
Hadi sasa Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki amechangia UWT Mifuko 120 ya Simenti yenye Thamani ya shilingi 2,760,000 Ngazi ya wilaya na mkoa kwa kutoa Mifuko 30 ya Simenti kila Wilaya Pamoja na kutoa shilingi Milioni 4,000,000 alizozitoa kwa UWT Kwa kutoa shilingi Milioni 1,000,000 kwa UWT Wilaya ya Mpanda,Tanganyika,Mlelen na UWT Mkoa kwaajili ya kusaidia ujenzi wa Nyumba za Watumishi wa UWT na kufanya jumla ya shilingi Milioni 6,760,000 alizo changia kwa UWT Mkoa wa Katavi kwaajili ya kusaidia ujenzi wa Nyumba za watumishi wa UWT Mkoa wa Katavi na Wilaya.