Mbunge Mavunde Akabidhi Mradi wa Shamba kwa Wanawake Wafanyabiashara Wadogo Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI MRADI WA SHAMBA KWA WANAWAKE WAFANYABIASHARA WADOGO DODOMA

▪️Mradi wa shamba la zabibu walenga kuwainua wafanyabiashara

▪️Wakinamama wampongeza kwa kuwainua kiuchumi

▪️Awatafutia soko la uhakika wa mazao yao

▪️Rais Samia apongezwa kwa miundombinu rafiki ya biashara kwenye masoko

📍Mpunguzi,Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amekabidhi mradi wa Shamba la zabibu kwa Wafanyabiashara Wanawake wa Masokoni (UWAWAMA) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa kongamano kubwa la Wafanyabiashara wanawake wa Masokoni wakati wa mkutano ulioongozwa na Mwenyekiti wa UWT Cde Mary Chatanda.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 20.02.2025 Mpunguzi,Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wanachama wa UWAWAMA.

“Rais Dkt. Samia S. Hassan amefanya kazi kubwa ya kujenga na kuboresha miundombinu ya masoko Jijini Dodoma kazi ambayo imechochea kukua kwa biashara na kuongezeka kwa kipato kwa wafanyabiashara wadogo.

Mradi huu wa Shamba la zabibu unategemewa kuongeza mapato na kutunisha mfuko wa wafanyabiashara wadogo.

Ni imani yangu kwamba mradi huu wa shamba utakuwa kichochea cha kukua kwa uchumi na mapato ya Umoja na kuongeza tija kubwa katika biashara zenu na nitahakikisha mnapata soko la uhakika wa mazao yenu.

Mradi huu ukawe nguzo kuu ya umoja, upendo na mshikamano na isiwe chanzo cha kupoteza umoja na kuruhusu mgawanyiko unaoweza kuleta athari kubwa ya ustawi wa umoja“Alisema Mavunde

Naye, Mwenyekiti wa UWAWAMA Bi. Anna James Mwita amemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo anavyowajali wakinamama na kuwainua kiuchumi na kuahidi kushirikiana kwa pamoja kuutunza na kuuendeleza mradi huo ili ulete tija kwa wakinamama wa masokoni sambamba na matumizi yenye tija ya fedha Tsh 10,000,000 kwa lengo la kutunisha mfuko wa Umoja.

WhatsApp Image 2025-02-20 at 19.59.57.jpeg
WhatsApp Image 2025-02-20 at 19.59.57 (1).jpeg
WhatsApp Image 2025-02-20 at 19.59.58.jpeg
WhatsApp Image 2025-02-20 at 19.59.58 (1).jpeg
WhatsApp Image 2025-02-20 at 19.59.58 (2).jpeg
WhatsApp Image 2025-02-20 at 19.59.59.jpeg
WhatsApp Image 2025-02-20 at 19.59.59 (1).jpeg
WhatsApp Image 2025-02-20 at 19.59.59 (2).jpeg
WhatsApp Image 2025-02-20 at 20.00.00.jpeg
WhatsApp Image 2025-02-20 at 20.00.00 (1).jpeg
 
MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI MRADI WA SHAMBA KWA WANAWAKE WAFANYABIASHARA WADOGO DODOMA

▪️Mradi wa shamba la zabibu walenga kuwainua wafanyabiashara

▪️Wakinamama wampongeza kwa kuwainua kiuchumi

▪️Awatafutia soko la uhakika wa mazao yao

▪️Rais Samia apongezwa kwa miundombinu rafiki ya biashara kwenye masoko

📍Mpunguzi,Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amekabidhi mradi wa Shamba la zabibu kwa Wafanyabiashara Wanawake wa Masokoni (UWAWAMA) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa kongamano kubwa la Wafanyabiashara wanawake wa Masokoni wakati wa mkutano ulioongozwa na Mwenyekiti wa UWT Cde Mary Chatanda.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 20.02.2025 Mpunguzi,Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wanachama wa UWAWAMA.

“Rais Dkt. Samia S. Hassan amefanya kazi kubwa ya kujenga na kuboresha miundombinu ya masoko Jijini Dodoma kazi ambayo imechochea kukua kwa biashara na kuongezeka kwa kipato kwa wafanyabiashara wadogo.

Mradi huu wa Shamba la zabibu unategemewa kuongeza mapato na kutunisha mfuko wa wafanyabiashara wadogo.

Ni imani yangu kwamba mradi huu wa shamba utakuwa kichochea cha kukua kwa uchumi na mapato ya Umoja na kuongeza tija kubwa katika biashara zenu na nitahakikisha mnapata soko la uhakika wa mazao yenu.

Mradi huu ukawe nguzo kuu ya umoja, upendo na mshikamano na isiwe chanzo cha kupoteza umoja na kuruhusu mgawanyiko unaoweza kuleta athari kubwa ya ustawi wa umoja“Alisema Mavunde

Naye, Mwenyekiti wa UWAWAMA Bi. Anna James Mwita amemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo anavyowajali wakinamama na kuwainua kiuchumi na kuahidi kushirikiana kwa pamoja kuutunza na kuuendeleza mradi huo ili ulete tija kwa wakinamama wa masokoni sambamba na matumizi yenye tija ya fedha Tsh 10,000,000 kwa lengo la kutunisha mfuko wa Umoja.

View attachment 3243909View attachment 3243910View attachment 3243911View attachment 3243912View attachment 3243913View attachment 3243914View attachment 3243915View attachment 3243916View attachment 3243917View attachment 3243918
Kampeni nzuri kuelekea Uchaguzi Mkuu!
 
Back
Top Bottom