Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. DKT. ALFRED KIMEA AAHIDI KUWAWEZESHA VIJANA WAJASILIMALI KOROGWE MJINI
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mhe. Dkt. Alfred Kimea, katika ziara yake aliyofanya jimboni amekutana na kufanya mazungumzo na vijana wajasiliamali wanaozalisha Kokoto, katika Kata ya Mtonga Mtaa wa Msambiazi.
Mhe. Dkt. Kimea, alitumia fulsa hiyo kusikiliza changamoto zinazowakabili vijana hao na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto hizo.
Pamoja na mambo mengine vijana hao wajasiliamali walimuomba Mbunge awapatie vitendea kazi vikiwemo Nyundo 40 na Machepe 40 ambayo ameahidi kuwaletea.
Aidha, Vijana hao walimshukuru na kumpongeza Mbunge wao kwa kazi anazofanya za kuwaletea maendeleo wananchi wa Korogwe Mji. Pia walimshukuru na kuwapongeza Mhe. Diwani Fransis Komba pamoja na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa zinazo fanyika.