Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. ABOOD ANAWAKARIBISHA WATANZANIA WOTE KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI MOROGORO
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini MHE. DKT. ABDULAZIZ M. ABOOD anawakaribisha Watanzania wote kutoka kila Eneo la Nchi yetu kwa ajili ya Sherehe za Mei Mosi zitakazofanyika tarehe 01.05.2023 Morogoro Mjini kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Mhe. Abood anawakaribisha kwa Upendo mkubwa na amesema Morogoro sisi ni wakarimu Sana, mkaribie na mjisikie mpo Nyumbani.
Aidha, Mhe. Abood amesema hata mkimaliza Shughuli za Mei Mosi muendelee kuwepo ili mtembelee Vivutio vya kitalii tulivyonavyo Kama Mlima Uluguru, Waterfalls, Kanisa la Kale, Makaburi ya Kale, Ndege wenye rangi za kuvutia, Wanyama wa aina yake n.k
Pia, Mhe. Abood anasema Msiache kutembelea Miradi mikubwa iliyotekelezwa na inazoyotekelezwa kwa Fedha alizozitoa MAMA Mhe. Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mathalani Vituo vikubwa vya Afya,
✅ Kituo cha Afya Tungi
✅ Kituo cha Afya Lukobe.
✅ Hospitali ya Wilaya
Shule Mpya za Sekondari Sita pamoja na Ofisi za Utawala, Maabara na Maktaba zake ambazo ni:-
✅ Mindu Sekondari
✅ Lukobe Juu Sekondari
✅ Mazimbu Sekondari
✅ Tungi Sekondari
✅ Mbuyuni Sekondari
✅ Mkundi Sekondari.
Ujenzi wa Zahanati sita za Kata, Miradi Mikubwa ya Maji Tank kubwa la Mgulu wa Ndege la Lita Milioni Mbili, Substation ya Maji, Miradi kamilifu ya Maji (Mradi wa Maji Bigwa-Kilakala, Kasi ya Ujenzi wa Mradi mkubwa wa SGR Morogoro
Mhe. Abood anawakaribisha Sana Sana, uwepo wenu ndani ya Jimbo la Morogoro Mjini, ni furaha kubwa Sana kwa Wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini.
KARIBUNI SANA