Mbunge Mpina ni mchumia tumbo tu, wala si mzalendo

Mbunge Mpina ni mchumia tumbo tu, wala si mzalendo

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Jamaa baada ya kuvuliwa uwaziri ndio amejifanya mtu wa kujenga hoja, ni baada tu ya kunyang'anywa tonge mdomoni.

Alibebwa na Hayati Magufuli Ila mfumo wa Mama samia umemtema. Mpina akubali kuwa kila mfumo una watu wake, laiti kama mfumo wa mzee msoga ungeendelea kuwepo hadi leo wengine tusingekuwa na hali hizi tulinazo leo. Lakini mbona tumekubaliana na hizi hali.

Hasira ya nini? ninachokielewa ni kuwa Mpina akipewa ulaji leo atakaa kimya, nipo nimekaa pale.

Soma==>>> Mpina kuwapeleka Mahakamani Waziri Bashe na Bodi ya Sukari kwa kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha Sheria
 
Ulitaka aje malaika mtakatifu asiye na dosari ndiyo akemee ubadhilifu na ufisadi hapa Tanzania na wala siyo watanzania wenyewe ( watu) amabao kimsingi hawakosi kasoro?

Kuna mahala popote alisema kuwa anapambana dhidi ya ufisadi kwa sababu alivuliwa uwaziri?
 
Alikuwa wapi kupambana Na ufisadi, Leo ndio ameuona ufisadi🤗🤗
 
Alikuwa wapi kupambana Na ufisadi, Leo ndio ameuona ufisadi🤗🤗
Hivi mtu mtenda dhambi akiamua kuwa mcha MUNGU akaanza kuhubiri na kukemea dhambi utamuuliza kuwa mbona ulikuwa mtenda dhambi mbona hukutuhubiri zamani ulikuwa wapi?

Jifunze kudeal na hoja siyo watu. Ukiweza hapo utapima ikiwa huyo mtu anaongea kwa manufaa yake au ya taifa lako🙏
 
Jamaa baada ya kuvuliwa uwaziri ndio amejifanya mtu wa kujenga hoja, ni baada tu ya kunyang'anywa tonge mdomoni, alibebwa Na magufuri Ila mfumo wa Mama samia umemtema ..Mpina akubali kuwa Kila mfumo Una watu wake, laiti kama mfumo wa mzee msoga ungeendelea kuwepo hadi Leo wengine tusingekuwa Na Hali hizi tulinazo Leo! Lakini mbona tumekubaliana Na hizi Hali....hasira ya nini?.. ninachokielewa ni kuwa Mpina akipewa ulaji Leo atakaa kimya..nipo nimekaa pale.
hii profile yako inaonesha kama kinyesi cha ng'ombe
 
Anachokizungumza mpina kinaweza kuwa ni kweli, lakini alikuwa wapi kuyazungumza haya Toka kipindi cha magu
Kila jambo Lina wakati wake,

Ni sawa Mimi nikuulize, kwanini thread hii umeileta Leo na Si Jana alipoongea Mpina!!

Jikite kwenye mada na HOJA za Mpina zijibiwe.

Habari ya kuzunguka HOJA Badala ya kujibu Si sawa!!
 
Acha majungu mkuu. Wewe mpinge Kwa hoja nasio brah brah zisizo na mantiki.
Zipi Sasa? Yeye mwenyewe fisadi tu,. Mpina leo atueleze wavuvi waliokuwa wanauwawa Na kufungwa magerezani wakikamatwa wakivua samaki kisiwa cha Rubondo chato walikuwa wanatumwa na nani??..ikumbukwe kwamba mpina enzi za magu alikuwa ndie waziri wa uvuvi.
 
Kila jambo Lina wakati wake,

Ni sawa Mimi nikuulize, kwanini thread hii umeileta Leo na Si Jana alipoongea Mpina!!

Jikite kwenye mada na HOJA za Mpina zijibiwe.

Habari ya kuzunguka HOJA Badala ya kujibu Si sawa!!
Hoja yangu iko pale pale mbunge Mpina ni mchumia Tumbo tu....hakuna mzalendo pale
 
Back
Top Bottom