Mbunge Msambatavangu Aitaka Serikali Kuweka Imani kwa Wawekezaji wa Ndani

Mbunge Msambatavangu Aitaka Serikali Kuweka Imani kwa Wawekezaji wa Ndani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

. MSABATAVANGU AITAKA SERIKALI KUWEKA IMANI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI

"Mmeanza kutubagua watanzania kwa kuwapa watu wenye uwezo wa fedha tusio na uwezo tusiwekeze kwakuwa miradi yetu ni midogomidogo, hao mabilionea ndiyo wawekeze 'This is not right' ni lazima watanzania wapewe fursa sawa ya kuwekeza biashara" - Mhe. Jesca Msambatavangu, Mbuge wa Iringa Mjini.

"Huu ni ubaguzi pamoja na kujenga imani kwa wafanyabiashara ni pamoja na kauli za viongozi kuzingatiwa, tunapoteza imani kwa wafanyabiashara kuwekeza Mheshimiwa Rais alisema kodi ya miaka mitano ya nyuma zisichajiwe lakini hakuna lolote lililofanyika, nchi hii Watanzania watamsikiliza nani? watu wanashindwa kuwekeza kwenye nchi yetu leo hii ahadi za viongozi hazitekelezwi" - Mhe. Jesca Msambatavangu, Mbuge wa Iringa Mjini.

"Mama ntilie wametafuta mitaji mnawachukulia Milioni mia sita kwemye akaunti zao kwamba wanadai kodi Hivi nchi hii kwani Tanzania hatusamehewi madeni na mataifa makubwa? Sisi tunakosa kuwasamehe mamantilie?" - Mhe. Jesca Msambatavangu, Mbuge wa Iringa Mjini.

"Iringa tuna migogoro miwili NFRA ambao huwa wananunua mahindi pale na Kuna watu CPB ambao nao wanazoezi la kununua mahindi kwenye kihenge chetu kinachoendelea pale NFRA hawajaanza kununua haya mazao na hawa CPB wakulima waliwalipa fedha tangu Mei 5 kwa maana ya kwamba walitaka kuuziwa mahindi ambayo yalikuwepo tayari yalishanunuliwa na bodi ya mazao mchanganyiko" - Mhe. Jesca Msambatavangu, Mbuge wa Iringa Mjini.

"NFRA hawana hela wangekuwa nazo kwanini CPB wanang'ang'ania fedha za wakulima kununulia mazao ili wawalipe mahindi wakulima wenyewe wakati NFRA wako pale wananunua? kwahiyo NFRA hawapo pale kununua ndiyo maana hata hao wakulima walioko pale wanaouza Mahindi bado wanaidai Serikali Kwasababu CPB nayo ni ya Serikali na NFRA ni ya Serikali pia" - Mhe. Jesca Msambatavangu, Mbuge wa Iringa Mjini
 

Attachments

  • FzPusSjX0AA88-T.jpg
    FzPusSjX0AA88-T.jpg
    40.9 KB · Views: 2
  • FzS6SSFXoAEufVz.jpg
    FzS6SSFXoAEufVz.jpg
    43.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom