Mbunge Msukuma Kasheku alilia wizi wa fedha za Umma

Mbunge Msukuma Kasheku alilia wizi wa fedha za Umma

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Kasheku amelilalamikia Bunge kwa nini haliwezi kutoa maamuzi ya kufanyiwa kazi.

Anapendekeza bora hoja bungeni zisipelekwe kuliko kupoteza muda.

Ktk clip inayosambazwa anatoa mifano kuwa kuna Mwizi ktk halimashari alipeleka jina lake kwa Waziri Bashingwa na hakuona mwitikio na hatua zilizofanyika.

Amewalalamikia Mawaziri kuwa wanapopokea malalamiko kutoka kwa wabunge hawayafanyii kazi.

Nasi watanzania tunajiuliza kama Wabunge hawasikilizwi je zile kero za wananchi mmoja mmoja nani atazisikiliza?

Je Spika Wa Bunge Dr Tulia Acksoni anajisikiaje anapokuwa anaongoza Bunge la namna hii lisilosikilizwa?
 
Kizimkazi mwenyewe hayupo atakua nje ya ofisi cku 5 na nina uwakika ataunga juu kwa juu taifa lingine.Atajuaje haya.
 
Nchi Ina hela sana,kodi zinakusanywa vilivyo,ila wezi ni wengi sana na wanajua namna wanavyolindana.Inakatisha tamaa sana.
 
Naam wizi hii nchi ni mwingi wa kutupa hata hao mjengoni kwa pesa wanazovuta na kile wanachofanya ni Day light Robbery.....
 
Kama wezi wakibainika wanahamishwa kituo badala ya kuchukuliwa hatua unategemea nini?

Kizimkazi anapalilia sana huu upigaji.
 
Back
Top Bottom