Kanamusi
Member
- Apr 9, 2020
- 22
- 65
Mbunge Musukuma sisi wakazi wa kanda ya ziwa hatukukutuma na hatujawahi kukuchagua kuwa msemaji wetu kwa jambo lolote.
Sisi wazee na watu wa kanda ya ziwa hatukukutuma kusema hayo unayoita mapigo ya kumjibu Antony Diallo na kama ulikuwa na nia ya kujibu mapigo ungemjibu kwa utashi wako au kwa niaba ya wananchi wa jimbo lako la Geita vijijini lakini sio kutuhusisha watu wa kanda ya ziwa kwenye maugomvi yako binafsi na kusema kwamba sisi ndio tumekutuma ukatusemee.
Sisi wazee wa kanda ya ziwa ni watu wenye busara na hekima, kama kuna jambo linaenda ndivyo sivyo tuna njia zetu za kuwasilisha maduku duku yetu ikiwemo kujisemea wenyewe na sio kutuma kijana mropokaji kama wewe.
Kuhusu kifo cha hayati Magufuli unasema tuliofiwa ni watu wa kanda ya ziwa. Kimsingi hii ni kauli ya kijinga kabisa kutolewa na kiongozi wa wananchi kama wewe kwa sababu Rais Magufuli hakuwa Rais wa kanda ya ziwa bali alikuwa ni Rais wa watanzania wote wa kanda za mikoa yote nchini. Sasa unaanzaje kusema kwamba tuliofiwa ni watu wa kanda ya ziwa pekee?
Huoni kama kauli yako inalenga kutugawa watu wa kanda ya ziwa na watu wa kanda zingine?
Kwa mara nyingine mbunge Musukuma usituhusishe tena wazee na watu wa kanda ya ziwa kwenye ugomvi wako binafsi wa kutafuta umaarufu wa kisiasa na sifa za kishamba na UKOME kabisa kutusemea kwa sababu hata sisi tuna midomo ya kujisemea.
Message sent & delivered