Wewe unamkataza musukuma kuwasemea watu wa ziwa mbona hatujakaa kikao kama wana ziwa tukakutuma wewe ukanushe hayo ya musukuma.kimsingi musukuma yuko sawa dialo kakosea sana.
Najaribu kuelewa hoja yako kuwa Musukuma yuko sawa, Diallo kakosea sana.
Nataka niwe upande wako.
Kwamba Diallo kakosea, Musukuma yuko sawa.
Musukuma anasema Diallo alikuwa Kambi ya Membe.
Musukuma anasema baada ya Uchaguzi, alifanikisha kikao cha Diallo kukutana na Magufuli.
Alifanikisha kikao hicho kwa sababu wote wawili, Magufuli na Diallo ni rafiki zake.
Baada ya Kikao hicho cha Diallo na Magufuli, tumeambiwa hapa JamiiForums na MwanaCCM Bw. Bollen Ngetti kwamba Diallo alimuita Bernard Membe aende kukutana nae, na aende na gari ya kukodi.
Bernard Membe hakwenda baada ya kupata taarifa kuwa huo ulikuwa mpango wa kumpoteza.
Kwamba Diallo kushindwa kufanikisha mpango huo, kulimuudhi sana Magufuli, ambaye aliamua Diallo apate madhira yaliyompata, ikiwa ni pamoja na kunyimwa malipo kwa kazi ya kuifanyia Kampeni CCM.
Hapa ninapata picha kuwa Mbunge Musukuma alikuwa sehemu ya kutaka kumpoteza Bernard Membe.
Na kwa kauli yake kuwa Kanda ya Ziwa ndiyo iliyofiwa baada ya Magufuli kuaga dunia, inaonyesha kuwa Ukanda ulikuwa uamuzi rasmi wa Utawala wa Magufuli ukipigiwa chapuo na watu wa aina ya Musukuma!
Siasa za Ukabila zitatufikisha wapi?