Mbunge Musukuma alivyoswekwa lupango baada ya kuongea hadharani kuwa Hayati Magufuli anamiliki hoteli


Umeiweka vizuri sana, huyu jamaa ni mnafiki sana na JPM alikua anamjua ndo mana hakuwahi kuwa na time nae.
 
Kweli mzee
 
Kuna watu wengi sana hawakupata tu fursa ya kwenda shule ila wako vizuri kichwani,Msukuma,Masoud kipanya nk.

Ila kuna wasomi wengi kama hawakwenda shule
bana weeee

hakupata fursa kivipi ?

shule zilikuwa bure

na shule nzuri ndo zilikuwa za serikali, za bure...

hao watu aidha hawakutaka kwenda shule...

au walikuwa wanafeli shule...

au Kasheku mwenyewe hakutaka kujiendeleza, maana alikuja kushika hela, kwa nini hakujisomesha ???

usimrembe rembe mtu ambae hakwenda shule enzi za Nyerere eti ana akili za shule bana...
 
Duh!...alizingua nini ?
Alilalamikiwa kutesa watu, kugonga watu misumari, kuwavunja. Jamaa akamwita dar akamtia ndani, siku chache tu baada ya kumfurahisha kukamata midolar, mzee hakujali.

Ambacho hatujui ni kwamba kuna mengi yalifanywa na watendaji tu wala hakuwatuma.
 
Ni kweli Msukuma ni kajamaa kanafiki Sana, kako after money, bendera fuata upepo.
 
Alilalamikiwa kutesa watu, kugonga watu misumari, kuwavunja. Jamaa akamwita dar akamtia ndani, siku chache tu baada ya kumfurahisha kukamata midolar, mzee hakujali.

Ambacho hatujui ni kwamba kuna mengi yalifanywa na watendaji tu wala hakuwatuma.
Vipi kifo Cha kamanda mawazo nani alihusika.
 
We jamaa Una akili sana
 
We jamaa Una akili sana
Nashukru sana kwa compliments zako
Hata hivyo naomba nitoe hoja hapa kwamba siyo kweli kwamba nina akili sana, kwa sababu kana ningekuwa hivyo, basi wewe usingeweza kugundua kuwa nina akili sana.

Kilichotokea kwenye post hii kati yangu mimi na wewe ni kwamba mimi nimejitahidi kuandika sawaswa kilicho kichwani kwangu, kukitoa kichwani kwangu na kukiweka kwenye karatasi ili na wengine waweze kukipata kama ninavyokifikiria kichwani kwangu na hivyo, baada ya wewe kuwa umekisoma, kikawiana na kile ambacho wewe mwenyewe huwa unacho kichwani mwako siku zote

Ningekuwa na akili sana, wewe usingeweza kugundua kuwa nina akili sana, lazima ningekupoteza mahali usingeelewa kitu.

Kile kilichopelekea wewe ukawa tempted kuniambia kuwa nina akili sana ni kwa sababu kile nilichoandika ndiyo kile ambacho kiko kwenye akili yako, kitu ambacho kina-prove kwamba fikra zako na zangu ziko sawa na hivyo akili zetu vile vile
 
Natokwa chozi kila nikiifikiria Tanzania ya miaka 100 ijayo, hali ya raia wengi wakati huo itakuwa ni mbaya sana kwasababu rasilimali nyingi zitakuwa kwenye miliki za watawala na familia zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…