Mbunge Musukuma asitake Kuhalalisha kuwa wenye Elimu ndogo wapendelewe, wasikilizwe sana na waonewe mno huruma na Watu kwa gharama ya kuwananga wasomi

Mbunge Musukuma asitake Kuhalalisha kuwa wenye Elimu ndogo wapendelewe, wasikilizwe sana na waonewe mno huruma na Watu kwa gharama ya kuwananga wasomi

Mimi kwa kua nimeishi maisha yangu ya mtaa kwa muda mrefu hasa baada ya elimu zangu zote na kwa kutambua hayo kila mmoja nampa nafasi yake naamini hawa wasomi wananafasi yao waheshimiwe lakini pia waelimike, kusoma sio kubeba GPA kubwa wakati kichwani wewe mwenyewe kujiendesha hauwezi, lakini pia tuwaheshimu hawa darasa la saba au ngumbalu maana maisha haya wasomi wetu wengi huomba kazi kwa hawa hawa kwani ndio wamehustle na washatoboa kitambo nadhani tukiishi kwa kiheshimiana na kupeana nafasi kila mmoja tutasonga mbele
 
Nadhani Msukuma anapoint nzuri tu sema ameshindwa kuisema vizuri...........ila ukikaa ukawa unasikiliza hoja za baadhi ya viongozi wetu unajiuliza huyu analevel yoyote ya elimu kweli? Asad Prof akaongezea kuwa asilimia kuwa ya Public servants ni incompitent........kuwa na elimu na kutumia vyema ni mambo ma2 tofauti
 
Lakini pia nahisi elimu yetu inawafanya watu wawe waoga hata wa kutetea kwa maarifa kile wanachoamini, na ndio maana inabidi serikali inabidi iuangalie mfumo mzima wa elimu yetu tujenge watu huru na sio watu wnaotegemea akili za wengine
 
Tatizo wanye elimu tokea wameingia kwenye siasa akili na professional zao wameziweka matakoni waoga kushauri, wanapitisha upuuzi tu, mimi ningeomba kwanza hawa prof na Dr, wenye masters na PhD watupishe tuwaamini degree na diploma kwa sasa tuone
 
Tatizo sio wasomi, ila aina ya wasomi tunaozalisha. Ukichukua form ya zamani ukalinganisha na mtu aliyetoka chuo utaona aibu. Ni wakati wa vyuo vyetu na serikali isisfikirie tu kuongeza idadi ya vyuo bali pia izingatie ubora wake ili wale wanaotoka pale waweze kuleta au kutumia elimu yao kwa manufaa ya jamii badala ya kulalamika hamna ajira.
 
Kwani mtu aliyesoma ana nini cha ziada na asiyesoma? Enzi za ukoloni wazungu hawakutaka tutoe mawazo yetu sisi watu weusi kwasababu walijua hatuna uwezo wa kufikiri mambo chanya na ndiyo maana walitufanya tuwe watumwa wao.
 
Nadiriki kutamka kwamba huyo alotajwa hapa pamoja na wenzie wa aina yake ni SABABU mojawapo ya nchi hii kutosogea KANANI kwa kasi stahiki yetu. Sio tu kwamba ni WAPAYUKAJI bila SUBSTANCE, uelewa wao wa ULIMWENGU huu unaohitaji nyongeza ya MAARIFA yapatikanayo baada ya ELIMU YAO YA CHEKECHEA ni finyu na TUSI. Chombo chetu cha kutunga sheria, BUNGE kingefaidika zaidi iwapo UWEZO ungepaishwa juu zaidi na wenye ELIMU nzuri na akili toshelezi. Ubingwa wa kupayuka payuka na vijimambo vidogodogo tena kiupashaji uelekezwe kwingine.

Nanukuu: "Lumpenproletariat"

Roughly translated as slum workers or the mob, this term identifies the class of outcast, degenerated and submerged elements that make up a section of the population of industrial centers. It includes beggars, prostitutes, gangsters, racketeers, swindlers, petty criminals, tramps, chronic unemployed or unemployables, persons who have been cast out by industry, and all sorts of declassed, degraded or degenerated elements. In times of prolonged crisis (depression), innumerable young people also, who cannot find an opportunity to enter into the social organism as producers, are pushed into this ...

ULUMPENI from a Marxist perspective, the case ya jamaa hao tajwa iko hivi:

In here demagogues and fascists of various stripes find some area of the mass base in time of struggle and social breakdown, when the ranks of the Lumpenproletariat are enormously swelled by ruined and declassed elements from all layers of a society in decay.

Ha ha!
 
Msukuma, na kishimba mimi nawaonaga wapo vizuri kwenye hoja zao ukilinganisha na hawa wasomi .
 
... yeye na kibajaji wana inferiority complex iliyo juu ya wastani. Sijui kwanini.
Dawa ya kuwapunguza hawa kenge kwenye chombo mhimu cha kuwakilisha wananchi ni ku-set academic qualifications kwa mtu kugombea nafasi nyeti kama ya ubunge. Dunia imebadilika sana tunahitaji smart and focused mind kuwawakilisha wananchi. Ifike mahali hawa darasa la tatu A walisaidie taifa kalika nafasi nyingine. SIYO UBUNGE. Kwa mtizamo wangu hata mwenyekiti wa mtaa anapaswa angalau awe amehitimu kidato cha nne.
Ova.
 
Dawa ya kuwapunguza hawa kenge kwenye chombo mhimu cha kuwakilisha wananchi ni ku-set academic qualifications kwa mtu kugombea nafasi nyeti kama ya ubunge. Dunia imebadilika sana tunahitaji smart and focused mind kuwawakilisha wananchi. Ifike mahali hawa darasa la tatu A walisaidie taifa kalika nafasi nyingine. SIYO UBUNGE. Kwa mtizamo wangu hata mwenyekiti wa mtaa anapaswa angalau awe amehitimu kidato cha nne.
Ova.
Kusoma na kuandika
 
Hoja za wasomi ndio zinazoplekea wenye elimu kudhalauliwa bungeni.
Hapana. Hoja za Musukuma, Kibajaji na Kishimba ni za burudani, siyo hoja za wanaojua mambo ya kisasa. Hoja za maendeleo ni kama zile za mchuano wa Muhongo na Kalemani kuhusu umuhimu wa vyanzo vya umeme, au Mdee na Kingu kuhusu hasara za kununua ndege, kila hoja imeshiba, inaulewa ulimwengu
 
Mimi kwa kua nimeishi maisha yangu ya mtaa kwa muda mrefu hasa baada ya elimu zangu zote na kwa kutambua hayo kila mmoja nampa nafasi yake naamini hawa wasomi wananafasi yao waheshimiwe lakini pia waelimike, kusoma sio kubeba GPA kubwa wakati kichwani wewe mwenyewe kujiendesha hauwezi, lakini pia tuwaheshimu hawa darasa la saba au ngumbalu maana maisha haya wasomi wetu wengi huomba kazi kwa hawa hawa kwani ndio wamehustle na washatoboa kitambo nadhani tukiishi kwa kiheshimiana na kupeana nafasi kila mmoja tutasonga mbele
Umesema vizuri kuwa asiyesoma anaweza kufanikiwa kiasi, lakini hawezi kutoboa kwenye ulimwengu wa kisasa bila msaada au kumwajiri aliyesoma
 
Muhongo mwenyewe alizungumza kwa maslahi finyu na yasiyokuwa na ukweli zaidi yakiashiria ,lengo na maslahi ya alikokuwa zamani
Lete ushahidi halisi, siyo wa kudhania. Aliongea kuwa tusitegemee bwawa la maji kama mwarobaini. Tuwekeze kwenye vyanzo vingine vya umeme pia, km gesi. Hayo yako kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM. Kaisome. Maslahi binfsi vipi.
 
Wenye elimu ndogo wapewe nafasi kuendesha nchi. Labda wako practical zaidi. Hawa wasomi wa kukariri wametuongoza toka uhuru lakini hakuna tulipofika. Haya maendeleo ni natural course tu ya mambo.
Kweli. Ukiona elimu ni shida, jaribu ujinga
 
Kwakweli kwa msomi hafai kuwa mwanasiasa.wakiwa wanasiasa akili inahama kabisa.hawawi wao.msukuma yuko sahihi wakati mwingine.
Mfano zile hela za escrow.wasomi walisimama kusema si hela za serikali.wakapigiana makofi.kaja JPM.kasema ni hela za serikali.hawahawa wasomi wakapiga makofi!bado tuwaheshimu?mhongo alimsapoti kikwete juu ya mradi wa gesi.kaja jpm.kasapoti umeme wa maji.JPM amefariki.anapinga huo mradi!mwanasiasa msomi nyeupe anaweza kusema ni nyekundu.usishangae.Lukuvi sio msomi kama unavyomjua.lakini kaimudu vizuri wizara.iliyowashinda wasomi kiwango cha profesa.si mnakubuka Tibaijuka?tupunguze mishahara kwenye siasa.ili
 
elimu zenyewe ndio hizi mapopoma mnakuja kuzionyesha kwa kujua kuongea kiingereza fasaha!!!

wacha akina kasheku wawachambe tu,hamjielewi.
 
Mimi ninachoamini mtu aliyesoma anajua vitu vingi vingi sana ambavyo hao wakina msukuma hawajui degree ni Elimu kubwa sana. Sijui wabunge wasomi Wanamuogopa kumjibu ndio maana anavimba kichwa na kuwa nanga, hakusoma tu akubali au arudi shule umri na umbo vinamruhusu.
Msomi kumjibu mtu kama msukuma itaamsha hasira za wajinga wengi sana. Yaani ni sawa na zile kelele za wanaopigania haki za wanawake. Haki za mtu kariba ya msukuma ina watetezi wengi sana.
 
Back
Top Bottom