Pre GE2025 Mbunge Musukuma atumia zaidi ya Tsh bilioni 1 kununua ambulance, gari la Polisi na kujenga kituo cha Polisi Geita Vijijini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Si kwa faida ya wananchi wake sasa ulitaka nani awanunulie
Pesa za mfuko wa jimbo ameshazila sana wacha arudishe fadhira
 
Miaka yote mitano amewaacha wanataabika weeeee, karibia na uchaguzi ndio kaamua kuwakumbuka ili wampe mitano mingine tena.
 
Msikilize kwanza ndo umdharau au umpe heshima yake
 
Yaani unasubiri mpaka mwaka wa uchaguzi halafu unatumia mkopo wa wabunge!! maajabu
 
Hii siyo kazi ya mbunge. Tena inaonyesha serikali ilivyoshindwa kuleta maendeleo. Yaani wakombe mabilioni ya fedha halafu watudanganye na kiduchu? Tunataka kuwe na mfumo endelevu wa kuhudumía wananchi na siyo hisani za mbunge.
 
Msikilize kwanza ndo umdharau au umpe heshima yake
Usidanganywe!! Hakuna mwanasiasa mwenye huruma na wananchi hadi atumie hela yake kwa ajili ya maendeleo au huduma kwa wananchi.
Maendeleo au huduma kwa wananchi hufadhiliwa na Serikali kuu, Halmashauri au wadau wa maendeleo na kisha wanasiasa hudandia waonekane ni wao ndo wamefanya. Kama hauko kwenye mfumo wa uongozi na utawala serikalini huwezi jua haya. Mtaendelea kudanganywa hadi mkome na kwa taarifa yako hao wanasiasa sio wajinga coz tukiwa nao kwenye vikao vya ndani na kukuwa hakuna camera wala waandishi wa habari ndo huwa tunajua wana akili sawasawa ila wakiwa majukwaani na kwenye camera coz wanajua watanzania wengi ni wajinga wajinga nao wanajifanya wajinga. Ni kama mwalimu wa darasa la kwanza kujifanya kuwa na tabia za kitoto angali si mtoto ili aendane nao watoto anaowafundisha, kadhalika na wanasiasa hujifanya wajinga ili waendane na wajinga wanaowaongoza
 
Leteni uthibitisho
 
Mbunge huyo pia amefichua kuwa gharama za mradi huo, ikiwemo ujenzi wa kituo cha Polisi cha kisasa kitakachokabidhiwa kwa Jeshi la Polisi, zimefikia zaidi ya shilingi bilioni moja.
Kutoka mfukoni mwake au?
 
Serikali inafanya kazi gani? Mshaurini alipe kodi vizuri tu mengine serikali itafanya
 
Serikali inafanya kazi gani? Mshaurini alipe kodi vizuri tu mengine serikali itafanya
Serikali hii hii au siyo?

Mi mwenyewe nataka kutoa fungu langu la kumi sitaki pesa ipitie serikalini,

Nitakwenda moja kwa moja kwa walengwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…