Tanzania Hakuna Tofauti Kati Ya Wasomi Na Ngumbalu Tukija Kwenye Mambo Mengi Sana.
Tukianzia Kwenye Utaalamu,Maamuzi Ya Kisiasa Na Maisha Ya Kawaida.
Hivi Mradi Wa Mwendokasi Unaendeshwa Na Malayman?
Temesa Pale Kuna Malayman?Wamekwenda Kukificha Kivuko Mombasa Sasa Hivi Wanakalibia Kumkabidhi Bakharesa Mradi.
Waziri Mzima Anasema Anamuomba Bakharesa Aende Apeleke Kwenye Vivuko Vingine Kama Mwanza Huko Zile Sea Tax Zake Inamaana Serikali Imeshindwa?Mimi Nawachukulia Wasomi Wa Tanzania Kama Watu Waliosomea Ujinga Na Wanastahiri Kubeba Lawama Za Umasikini Wa Nchi Hii.
We Angalia Hata Kwenye Sskta Ya Michezo Wazee Wa Darasa La Nne La Mkoloni Waliweza Kujenga Majengo Kwa Timu Za Simba Na Yanga Ila Hawa Wa MaPhd Wa Sasa Wamebaki Kudandia Viwanja Vya Watu Na Kujisifu.
Hata Mleta Mada Ni Mmoja Wa Mambulula Wa Utumwa Wa Simba Na Yanga Wakizindua Vitambaa Vyao Wenyewe Wanaita Jezi Wanapanga Mstari Kwenda Kutajirisha Watu Binafsi Wakiziacha Timu Zao Bado Omba Omba.Bora Ya Msukuma Kuliko Wasomi Mia Moja Wa Tanzania Kwanza Ametengeneza Ajira Kwa Watanzania Wenzake Ana Kila Sababu Ya Kutamba Ila Wewe Na Vyeti Vyako Kila Siku Unachungulia Ajira Portal ,Kusujudia Wanasiasa Kwa Nyimbo Na Mapambio.
Hovyo Kabisa.
Kapingana sana na wewe.
Ukifuatilia sana utagundua kuwa mfumo ndio mbaya sio wasomi .
Mfumo huwezi kupingana nao peke yako ukaishinda labda uwe Nabii au mteule wa Mungu Kama Tundu Lisu.
Fuatilia ujiulize ni kwanini wanakataa kuwapa mkopo wanafunzi waliosoma Shule binafsi kama seminari ili wasome vio vikuu na hata kupata scholarship nje ya nchi?
Kwa nini Walipotaka kuuza kila kitu walianza kwanza kufuta masomo ya biashara na kilimo mashuleni! ?
Kwa nini walifuta ufaulu wa masomo ya dini kujiunga na vyuo vikuu kwenye fani za sheria ,socialogy, social work n.k wakati Masomo ya dini kwa upana wake ni msingi wa sheria na haki na ustawi wa jamii bora yenye usawa?
Matokeo yake watu wengi waliokuwa wana hofu ya Mungu na waliokua hawapendi ufisadi kuanzia mashuleni wanaonekana kama watu hatari katika kupinga ufisadi na uhuni mwingi katika nafasi walizonazo kwenye jamii.
Kilichofuata ni nini ? Ni kuwa na wasomi wanapeana Connection kwenye mabaa , starehe ,uzinzi n.k. Ili wapate pesa za kulewa na kufanya starehe zote hizo ni lazima wapate pesa nyingi kila siku na walewe kila siku na kula nyama choma na kiti moto . Watazipata wapi ? Bila shaka ni kulingana na urefu wa Kamba zao. Hapo hakuna cha msomi wala maamuma wote ni kutafuna kulingana na urefu wa kamba .Mwenye kamba ndefu starehe atafanyia Dubai ,Zanzibar , Canada n.k.
Watu wa starehe kamwe hawawezi kufanya kazi za kujiajiri labda kama wanamali za urithi lakini sio from zero to hero . Ndio maana Wapemba wanatajirika kuanzia chini kabisa kwa sababu ya kujiepusha na starehe na ulevi . Huwezi kuuza genge la nyanya ukapata faida ya sh. 10000 halafu jioni una kaa kwenye baa na marafiki na kunywa yote .Labda kama unauza bangi pia na unga !
Mfumo umeifanya jamii kuwaamini wahuni ,wahalifu na mafisadi na kuwapa heshima kubwa kuanzia kwenye nyumba za ibada mpaka mitaani . Sasa wasomi nao wanatumia udhaifu huo kupiga pesa za umma.