Mbunge Musukuma nae ni kati ya watunga sera na sheria za nchi yetu?

Upo sahihi saana elimu ya Tanzania haina Tija hivyo vi degree vyao ni kujisifu tu na kuiba, na ubishi usikua na maana haviwezi kusimamia chochote ety wasomi😡😡😡😡 Yani tz mtu akiwa na degree tu aseee basi shida
 
Bado msukuma anawakilisha jamii kubwa ya watanzania wajinga mkimfunga msukuma hao wajinga atawawakilisha nani
Huko anapigiwa makofi tena kwa nguvu na wanamuona ndiye msomi kwao
Siyo kila ambaye hajasoma hawezi kujenga hoja
Isipokuwa yaweza tokea

Narudia msukuma anawakilisha kundi kubwa sana la ujinga Tanganyika
 
😁Huu msumari kweli ni wa Inch 9
 
Na
analipwa mshahara mkubwa kuliko IGP na polisi wote na Magereza wote na Karibu Wanajeshi wote . Halafu eti uchaguzi ukifika dola inabeba masanduku ya wizi wa kura ili ashinde.

Kodi za watanzania zinaliwa na genge la Wahuni.
 
Wawakilishi wetu wanapaswa kutokana Kila kundi katika jamiii yetu Kama wasomi, walemavu, wazee, vijana, ke, nakadhalika mchanganyiko huo huunda bunge letu tukufu na hoja hujibiwa kwa hoja.
 
Kapingana sana na wewe.

Ukifuatilia sana utagundua kuwa mfumo ndio mbaya sio wasomi .

Mfumo huwezi kupingana nao peke yako ukaishinda labda uwe Nabii au mteule wa Mungu Kama Tundu Lisu.
Fuatilia ujiulize ni kwanini wanakataa kuwapa mkopo wanafunzi waliosoma Shule binafsi kama seminari ili wasome vio vikuu na hata kupata scholarship nje ya nchi?
Kwa nini Walipotaka kuuza kila kitu walianza kwanza kufuta masomo ya biashara na kilimo mashuleni! ?
Kwa nini walifuta ufaulu wa masomo ya dini kujiunga na vyuo vikuu kwenye fani za sheria ,socialogy, social work n.k wakati Masomo ya dini kwa upana wake ni msingi wa sheria na haki na ustawi wa jamii bora yenye usawa?
Matokeo yake watu wengi waliokuwa wana hofu ya Mungu na waliokua hawapendi ufisadi kuanzia mashuleni wanaonekana kama watu hatari katika kupinga ufisadi na uhuni mwingi katika nafasi walizonazo kwenye jamii.

Kilichofuata ni nini ? Ni kuwa na wasomi wanapeana Connection kwenye mabaa , starehe ,uzinzi n.k. Ili wapate pesa za kulewa na kufanya starehe zote hizo ni lazima wapate pesa nyingi kila siku na walewe kila siku na kula nyama choma na kiti moto . Watazipata wapi ? Bila shaka ni kulingana na urefu wa Kamba zao. Hapo hakuna cha msomi wala maamuma wote ni kutafuna kulingana na urefu wa kamba .Mwenye kamba ndefu starehe atafanyia Dubai ,Zanzibar , Canada n.k.
Watu wa starehe kamwe hawawezi kufanya kazi za kujiajiri labda kama wanamali za urithi lakini sio from zero to hero . Ndio maana Wapemba wanatajirika kuanzia chini kabisa kwa sababu ya kujiepusha na starehe na ulevi . Huwezi kuuza genge la nyanya ukapata faida ya sh. 10000 halafu jioni una kaa kwenye baa na marafiki na kunywa yote .Labda kama unauza bangi pia na unga !

Mfumo umeifanya jamii kuwaamini wahuni ,wahalifu na mafisadi na kuwapa heshima kubwa kuanzia kwenye nyumba za ibada mpaka mitaani . Sasa wasomi nao wanatumia udhaifu huo kupiga pesa za umma.
 
Wako pamoja na Professor Mkenda, Kabudi, Ndakidemi, Dr Biteko, Dr Jafo
 
Na hana utajiri wowote defaulter mkubwa anakopa mabenki na halipi. Hakuna mtu mwenye credit reference chafu TZ kama Joseph kasheku
 
Learn to be constructive

Next time weka mtazamo wako kwa hoja, tathmini chanya ya mchango weka, kisha weka mapungufu ya mtazamo wake, tazama hybrid thinking hio three angle thinking approach.

Put your submissions in terms of meaningful and constructive critics.

Not any person is an all inclusive master of solutions to issues.

We need to shape how we look at things holistically with global reflections, we're not an island.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…