Mbunge Nancy Nyalusi: Serikali Imeleta Bilioni 1.8 ya Miradi ya Maendeleo Kata ya Kising'a, Iringa

Mbunge Nancy Nyalusi: Serikali Imeleta Bilioni 1.8 ya Miradi ya Maendeleo Kata ya Kising'a, Iringa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE NANCY NYALUSI: SERIKALI IMELETA BILIONI 1.8 YA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA KISING'A, IRINGA

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Mhe. Nancy Nyalusi amezungumza katika Kata ya Kising'a Wilaya ya Iringa na amewataka wananchi kutembea kifua mbele na kujivunia uwepo wa Serikali sikivu kwani katika kipindi kifupi tayari fedha Shilingi Bilioni 1.8 zimepelekwa kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye kata hiyo.

Mhe. Nancy Nyalusi amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwa sikivu hasa katika kushughulikia kero mbalimbali katika jamii.

Amesema pamoja na kwamba miradi ya mendeleo mkoani Iringa ni mingi lakini Serikali kwa upekee katika Kata ya Kising'a peke yake imeleta Shilingi Bilioni 1.8.

Amesema kiasi hicho kikubwa cha fedha kimekwenda kutatua changamoto katika Sekta za Elimu, Maji na Afya kwenye kata hiyo.

"Mnaweza kuona ni jinsi gani Serikali imedhamilia kumaliza changamoto kwenye maeneo kadhaa hususani kwenye elimu, afya na maji kwani tayari katika muda mfupi imetoa Shilingi Bilioni 1.8" - Mhe. Nancy Nyalusi.

Mhe. Nancy Nyalusi amesema: "Wakina mama Mhe. Rais anapambana sana usiku na mchana kwa ajili yetu, keki ya Taifa ni ndogo lakini kwa upendo mkubwa Rais wetu anagawa kidogo kidogo ili kila kijiji, kila kata nchini ipate fedha kwa ajili ya maendeleo, katika kipindi kifupi cha miaka 3 ya uongozi wake kila kijiji kimepata mradi"

Mhe. Nyalusi amesema kufuatia juhudi na upendo huo unaonyeshwa na Rais, wananchi wana kila sababu yakuona wana wajibu wa kumsaidia kazi lakini pia wakati wote kumuombea afya njema wakati wote.

"Juhudi zote hizo sio kwetu tu watu wa Iringa bali ni kwa nchi nzima na ikumbukwe tupo watu Milioni 61 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi, hakika Rais wetu anastahili pongezi" - Mhe. Nancy Nyalusi

Katika hatua nyingine leo katika ziara hiyo Mhe. Nancy Nyalusi pia ametembelea Shule ya Msingi Igingilanyi ili kuona jinsi fedha Shilingi Milioni 5 aliyotoa shuleni hapo imetumiwaje.

Akiwa shuleni hapo Mhe. Nyalusi amesema ameridhishwa na jinsi fedha hiyo ilivyotumika na kuahidi kuendelea kuchangia maendeleo shuleni hapo na kijijini hapo.

Aidha, katika mkutano wake wa hadhara Mbunge huyo wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa amezungumza na vikundi mbalimbali vya maendeleo vya akina mama wajasiliamali na kuwaeleza dhamira yake ya kuwatafutia fedha kwa ajili ya kutunisha mifuko wa vikundi hivyo ambazo zitatumika kama mitaji wa wakinamama hao.

Mhe. Nyalusi yupo katika ziara ya kazi ya siku 8 mkoani Iringa ambayo kaianza leo mapema kata ya Kising'a.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-07-18 at 12.14.45.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-18 at 12.14.45.jpeg
    429.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom