Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
MBUNGE NDAISABA RUHORO AKICHANGIA HOJA KATIKA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI BUNGENI JIJINI DODOMA
Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara Akichangia Bungeni Jijini Dodoma wakati Hotuba ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 ikiendelea kujadiliwa Bungeni Dodoma.
Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusambaza huduma ya umeme katika Vijiji vyote vya Jimbo la Ngara na Vijiji vyote Tanzania pamoja na kujenga miradi ya umeme ukiwamo mradi wa umeme wa Rusumo
Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ameiomba Wizara ya Nishati kuongeza na kuzidi kusambaza umeme katika Vitongoji vyote kuelekea 2030 Vitongoji ili vingi vifikiwe na huduma ya umeme.
Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ameiomba Wizara ya Nishati kufanya maboresho ya kuletwa Transifoma zenye uwezo mkubwa kwani transifoma za KVA50 zina uwezo mdogo wa kuhudumia wananchi wachache na amependekeza transifoma za KVA100 na KVA200 zinaweza maliza tatizo hilo.
Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ameiomba Wizara ya Nishati, TANESCO na REA kuleta mitungi ya gesi inayoenda sambamba na matumizi ya majiko ya umeme majumbani pia kusambaza vifaa vinavyotumia umeme kwa bei nafuu.
Mwisho, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ametoa taarifa ya Vijiji vitano katika Jimbo la Ngara ambavyo Transifoma zimeharibika na hivyo kuathiri huduma ya umeme katika Vijiji hivyo vya Mkalinzi, Kititiza, Mkubu, Mmilamila na Muganza na kuiomba Wizara Kuja na Mwarobaini wa tatizo hilo.