Mbunge Neema Lugangira(Viti Maalum) ashauri Biashara za Mtandaoni kuanza kutozwa Kodi

Mbunge Neema Lugangira(Viti Maalum) ashauri Biashara za Mtandaoni kuanza kutozwa Kodi

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi Mheshimiwa Neema amehoji kwa nini biashara za mtandaoni hazitozwi kodi kama biashara nyingine zinazofanyika nje ya mtandao. Mbunge huyo amenukuliwa akisema "Biashara ikifikia mauzo ya 4m, TRA wanatoza Kodi ya 100k/mwaka.

Biashara ikifikia mauzo ya 100m wanasajiliwa VAT na wanatozwa Kodi kulingana na Faida. Kwanini biashara za mtandaoni zisitozwe Kodi hata zikifikia mauzo stahiki? TUJADILI Online vs Offline ✍".

Pia, soma:

1). Dkt. Ndugulile: Kutoza kodi Mapema kwenye Biashara za mitandaoni kutaua ajira za Vijana wengi na kudumaza e-Commerce

Yuko sahihi kabisa; Marekani siku hizi majimbo mengi yanatoza kodi mauzo yote ya mitandaoni. Kampuni kama Amazon, maduka yake ni ya mtandanoni na ndiyo yenye mauzo mengi kuliko kampuni yoyote.

Sasa iwapo wa offline mwenye mauzo kidogo analipa kodi, iweje online mwenye mauzo mengi asilipe kodi.

Tatizo sasa litakuwa kwenye uhakiki wa hizo biashara za mtandaoni
 
Kuna tofauti ya kutafuta wateja mtandaoni na kufanya biashara kwa njia ya mtandao. Watanzania wengi wanatafuta wateja mtandaoni na sio kufanya biashara mtandaoni.

Unakuta mtu ana duka lake Kariakoo na anawapa vijana bidhaa watagute wateja mtandaoni kwa lengo la kuiuza. Kwa mfano huo utasema hiyo ni Online Business?

Ni muhimu kuielewa kwanza dhana ya e-Business kabla ya kufikiria kulipa Kodi.
 
Yuko sahihi kabisa; Marekani siku hizi majimbo mengi yanatoza kodi mauzo yote ya mitandaoni. Kampuni kama Amazon, maduka yake ni ya mtandanoni na ndiyo yenye mauzo mengi kuliko kampuni yoyote. Sasa iwapo wa offline mwenye mauzo kidogo analipa kodi, iweje online mwenye mauzo mengi asilipe kodi.

Tatizo sasa litakuwa kwenye uhakiki wa hizo biashara za mtandaoni
Mkuu unachokieleza hapa ni tofauti na kile anachomaanisha mheshimiwa mbunge.
 
Mbona yeye mshahara wake haukatwi kodi yuko kupiga kelele.

Mtandaoni ni sehemu ya kukutanisha muuzaji na mnunuaji, akilipa kwa njia ya simu kachangia VAT pamoja na tozo. Wanataka nini kingine.

Akifika dukani au ofisini anachangia halmashauri na kodi zingine.

Jiwe alilikosea sana ili taifa kuweka watu hao madarakani
 
Yuko sahihi kabisa; Marekani siku hizi majimbo mengi yanatoza kodi mauzo yote ya mitandaoni. Kampuni kama Amazon, maduka yake ni ya mtandanoni na ndiyo yenye mauzo mengi kuliko kampuni yoyote. Sasa iwapo wa offline mwenye mauzo kidogo analipa kodi, iweje online mwenye mauzo mengi asilipe kodi.

Tatizo sasa litakuwa kwenye uhakiki wa hizo biashara za mtandaoni
Tanzania hakuna biashara ya mtandao ila mitandao ni mahali pa kukutanisha wanunuzi na wauzaji.

Je ni platform gani Tanzania ambayo analipia bidhaa online?

Kupatana

Zoom

Jiji

Facebook ads

Instagram Ads

Whatsapp status

Show me kwenye hizo platforms zote ni ipi mtu analipia hela kwenye platform?

Mambo ya kusema Mbunge awe ameishia class 7 ndio tunapata hoja kama hizi.

Anachokitaka hakitekelezeki.
 
Mkuu unachokieleza hapa ni tofauti na kile anachomaanisha mheshimiwa mbunge.
Nimemwelewa hivyo; angalia juzi nilinunua kitu amazon.com, bado nililipia tax. Vile vile, kwa Amazon kuniuzia kitu mtaani kwangu, serikali ya mtaa nayo inapata kodi ya biashara kutoka Amazon.

Kwa hiyo serikali inapata kodi mbile: ile ya mauzo kutoka kwangu mnunuzi, na kodi ya biashara kutoka Amazon muuzaji, ingawa ile % ya kodi ya biashara ni ndogo sana kwa biashara za online kulinganisha na zile za offline, lakini bado wanalipa.

1646916194502.png
 
Nimemwelewa hivyo; angalia juzi nilinunua kitu amazon.com, bado nililipia tax. Vile vile, kwa Amazon kuniuzia kitu mtaani kwangu, serikali ya mtaa nayo inapata kodi ya biashara kutoka Amazon. Kwa hiyo serikali inapata kodi mbile: ile ya mauzo kutoka kwangu mnunuzi, na kodi ya biashara kutoka Amazon muuzaji, ingawa ile % ya kodi ya biashara ni ndogo sana kwa biashara za online kulinganisha na zile za offline, lakini bado wanalipa.

View attachment 2145767
Tanzania kuna Platform gani inayofanania na Amazon?
 
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi Mheshimiwa Neema amehoji kwa nini biashara za mtandaoni hazitozwi kodi kama biashara nyingine zinazofanyika nje ya mtandao. Mbunge huyo amenukuliwa akisema "Biashara ikifikia mauzo ya 4m, TRA wanatoza Kodi ya 100k/mwaka.

Biashara ikifikia mauzo ya 100m wanasajiliwa VAT na wanatozwa Kodi kulingana na Faida. Kwanini biashara za mtandaoni zisitozwe Kodi hata zikifikia mauzo stahiki? TUJADILI Online vs Offline ✍".

View attachment 2145753
Viti maalum vifutwe kwa manufaa ya taifa
 
Back
Top Bottom