No! hujui unalosema wewe. Tena kadri unavyoendela na mjadala ndipo unazidi kujionyesha unapinga jambo usilojua. Unarukaruka kila pembe bila kuwa na coherent argument. Usilaumu bila kujua unatetea nini
Elewa hivi:
(1) Ukiagiza bidhaa yako popote dunini itabidi ulipie kodi ya forodha kwa viwango vilivyowekwa na serikali. Haiyo haijalishi kama bidhaa hiyo ni kwa matumizi yako binafsi au ni kwa ajili kuuuza. Hiyo kodi ya forodha ni kitu kimoja na inalipwa kwa bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nje tu.
(2) Ukiuza bidhaa yoyote, bila kujali bidhaa hiyo imetoke wapi, unatakiwa ulipie kodi ya mauzo.
(3)Sasa iwapo unauza biadha uliyonunuea kutoka mtu mwngine aliyoegiza bidhaa hiyo kutoka nje, ni lazima msululu wa kodi hizo uwepo. Hata hivyo, serikali imeweka utaratibu wa kuondoa sehemu ya kodi hizo kwa resellers lakini mfumo unatakiwa uwe hivyo.
Kuwa na leseni ya kufanya biashara ni kitu tofauti kabisa na kodi. Leseni ni kibali cha serikali kukuruhusu wewe kufanya biashara, na kodi na malipo serikali yatokanyo na mauzo. Unbaweza kuwa na leseni lakini usiwe na mauzo, hivyo usilipe kodi, lakini huwezi kufanya mauzo bila kuwa na leseni.