Mbunge Neema Lugangira(Viti Maalum) ashauri Biashara za Mtandaoni kuanza kutozwa Kodi

Si vyote vinafanyika Marekani vifanyike Bongo. Mtaua ubunifu na mitaji. Fanyeni study kwanza!
Kuna vitu ambavyo ni natural lazima tufanane. Kulipa kodi serikalini ni natural contract kati ya raia na serikali, hatuwezi kukwepa.
 
Mhona Marekani tangu zamani Rais hateui tume ya uchaguzi na hatujaiga hilo?
marekani wanafuata katiba ya Marekani, na Tanzania tunafuata katiba ya Tanzania. Ila contract kati ya serikali na raia sehemu yoyote ni kuwa raia analipa kodi serikalini. Dunia nazima raia hulipa kodi serikalini labda kama serikali imesamehe tu.
 
Sasa hiyo kutanganziana facebook au jamii forums halafu mnauziana pembeni hiyo siyo online business. Ni kama kutangaza gazetini au redioni halafu manauziana pembeni, hawezi kuwa onradio business au in newsapepr business. Mimi ninazungumzia zile online business ambazo zinazua bidhaa online, yaani malipo yanafanyika online, na nimetoa mifano yake kwenye post mojawapo huko nyuma.
Tanzania ni ngapi hizo? Na hazilipi kodi how? Mfano moja ya requirement ya payment gateway ya M-PESA ni kusajiliwa as a business in Tanzania which means una TIN na mauzo yanakuwa tracked as a platform ni ngumu kuepuka kodi..., huyu anazungumzia wale wa insta na WhatsApp ambao mimi nawaita Machinga wa Online mwisho wa siku hujui kama kauza au hajauza au mtu anapost kuuza gari Zoom au Kupatana
 
Kuna vitu ambavyo ni natural lazima tufanane. Kulipa kodi serikalini ni natural contract kati ya raia na serikali, hatuwezi kukwepa.
Wewe jamaa upo obsessed na kodi bila kujali unamtozaje mtu hiyo kodi. Wajengeeni uwezo kwanza wawe na biashara rasmi na endelevu then ndo mtoze hizo kodi zenu.

NB: Je, mapato yote ya Wabunge yanatozwa kodi? Kipi cha uhakika; biashara ya mitandao au mapato ya wabunge??
 
Nimemwelewa hivyo; angalia juzi nilinunua kitu amazon.com, bado nililipia tax. Vile vile, kwa Amazon kuniuzia kitu mtaani kwangu, serikali ya mtaa nayo inapata kodi ya biashara kutoka Amazon. Kwa hiyo serikali inapata kodi mbile: ile ya mauzo kutoka kwangu mnunuzi, na kodi ya biashara kutoka Amazon muuzaji, ingawa ile % ya kodi ya biashara ni ndogo sana kwa biashara za online kulinganisha na zile za offline, lakini bado wanalipa.

View attachment 2145767
Hebu tutajie biashara ya mtandaoni ya hapa 255?tutofautishe kuuza na kutangaza biashara mtandaoni
 
Tanzania ni ngapi hizo? Na hazilipi kodi how? Mfano moja ya requirement ya payment gateway ya M-PESA ni kusajiliwa as a business in Tanzania which means una TIN na mauzo yanakuwa tracked as a platform ni ngumu kuepuka kodi..., huyu anazungumzia wale wa insta na WhatsApp ambao mimi nawaita Machinga wa Online mwisho wa siku hujui kama kauza au hajauza au mtu anapost kuuza gari Zoom au Kupatana
Umeongea point mkuu hawa machinga wa online ningumu kuwapata ili uwatoze kodi,gateways bila kusajili biashara ningumu nashukuru umelizungumzia vizuri watu wengi wanashindwa kutofauti online business na platform za kizushi mtu kafungua group kwenye whatspp au FB mtu anakuambia ni online business?
 
Viti maalum vifutwe sasa, waanze kugombea ili wapatikane watu wenye akili kidogo huko bungeni. Shujaa alituharibia nchi sana.
 
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi Mheshimiwa Neema amehoji kwa nini biashara za mtandaoni hazitozwi kodi kama biashara nyingine zinazofanyika nje ya mtandao. Mbunge huyo amenukuliwa akisema "Biashara ikifikia mauzo ya 4m, TRA wanatoza Kodi ya 100k/mwaka.

Biashara ikifikia mauzo ya 100m wanasajiliwa VAT na wanatozwa Kodi kulingana na Faida. Kwanini biashara za mtandaoni zisitozwe Kodi hata zikifikia mauzo stahiki? TUJADILI Online vs Offline [emoji871]".

View attachment 2145753
Hivi anajua Anacho Kinena?
 
Tanzania ni ngapi hizo? Na hazilipi kodi how? Mfano moja ya requirement ya payment gateway ya M-PESA ni kusajiliwa as a business in Tanzania which means una TIN na mauzo yanakuwa tracked as a platform ni ngumu kuepuka kodi..., huyu anazungumzia wale wa insta na WhatsApp ambao mimi nawaita Machinga wa Online mwisho wa siku hujui kama kauza au hajauza au mtu anapost kuuza gari Zoom au Kupatana
Machinga siyo biashara kwani haina leseni na hivyo haikatwi kodi, ni vivyo hivyo kutangaziana instagram na kuuziana mtu na mtu siyo biashara kwa vile haina leseni.
Hebu tutajie biashara ya mtandaoni ya hapa 255?tutofautishe kuuza na kutangaza biashara mtandaoni
Baadhi yake ni kama ifuatavyo

Wewe jamaa upo obsessed na kodi bila kujali unamtozaje mtu hiyo kodi. Wajengeeni uwezo kwanza wawe na biashara rasmi na endelevu then ndo mtoze hizo kodi zenu.

NB: Je, mapato yote ya Wabunge yanatozwa kodi? Kipi cha uhakika; biashara ya mitandao au mapato ya wabunge??
Hiyo ya wabunge kutokulipa kodi au kulipwa posho juu ya mishahara kwa kazi waliyoomba nimewahi kuilalamikia sana pia kuwa siyo sahihi. Anapogombea awe anajua mashahara wa kazi hiyo ni upi na apokee mshahara huo huo hadi anamaliza kipindi chake. Nyongeza ya mishahara ya wabunge inapofanywa isiwe effective mpaka baada ya uchaguzi. Kwa kosa la wabunge kutokulipa kodi haina maana kuwa kodi nyingine pia zisilipwe. Ni afadhali kudai wabunge pia walipe kodi, lakini siyo kukataza wengine wasilipe kodi kwa vile wabunge hawalipi kodi.
 
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi Mheshimiwa Neema amehoji kwa nini biashara za mtandaoni hazitozwi kodi kama biashara nyingine zinazofanyika nje ya mtandao. Mbunge huyo amenukuliwa akisema "Biashara ikifikia mauzo ya 4m, TRA wanatoza Kodi ya 100k/mwaka.

Biashara ikifikia mauzo ya 100m wanasajiliwa VAT na wanatozwa Kodi kulingana na Faida. Kwanini biashara za mtandaoni zisitozwe Kodi hata zikifikia mauzo stahiki? TUJADILI Online vs Offline ✍".

View attachment 2145753
Mvuvi akisifiwa, ngoma ikipigwa Sana, ukiinuliwa na wanadamu... Atajikwaa muda c mrefu.
 
Machinga siyo biashara kwani haina leseni na hivyo haikatwi kodi, ni vivyo hivyo kutangaziana instagram na kuuziana mtu na mtu siyo biashara kwa vile haina leseni.

Baadhi yake ni kama ifuatavyo

Nfano kama hawa Buy or Sell Anything Yourself With Either Auction or Without Auction. platform yao iko vizuri kuna siku nitumia platform yao kufanya biashara na mtu nikalipa pesa bank nikapata mzigo wangu, je bila kulipa kodi bank watakubali ufungue account ?Sijui mbunge anazungumza online business gani.
 
Unaweza kuwa na account benki na usilipe kodi. Inategemea kama hiyo biashara yako ya kwenye mtandao ina leseni au haina; na inawezekana yeye anaongelea biashara za namna hiyo ambazo hazina leseni.
 
MKuu sijakuelewa umenipoteza kidogo unawezaje kufungua account ya biashara bank bila tax clearance certificate ,Lesen, TIN, memorandum na certificate of incorporation ?
 
Back
Top Bottom