Mbunge Neema Lugangira(Viti Maalum) ashauri Biashara za Mtandaoni kuanza kutozwa Kodi

Mbunge Neema Lugangira(Viti Maalum) ashauri Biashara za Mtandaoni kuanza kutozwa Kodi

Kwa hiyo ni biashara gani ya mtandao anayozungumzuia ambayo anataka ilipiwe kodi?

Ninajua kuwa Tanzania kuna platform kadhaa za aina ya Amazon zinazofanya mauzo online; labda sema kuwa wewe binafsi huzifahamu lakini usiseme kuwa hazipo.

Baadhi yake ni kama ifuatavyo

Sasa labda nikuongezee tuu kuna jamaa wanaitwa laptop city ukitaka kununua kitu wakati wa ku check out VAT inaongezeka..sasa kimsingi huyu mama anataka watu wa instagram na facebook walipe kodi yani ulipe kodi kwa kutafuta wateja online...🤣🤣🤣🤣 hizo ulizoziwema sijajaribu ila nadhani unaweza kuta mwishoni VAT inaongezeka
 
Hako kadada kanatafuta sana uteuzi

Mshahara wake tu sijui kama unakatwa kodi
 
Kama wabunge hawalipi kodi na wengine nao wasilipe na kinyume chake.
Hiyo ndo misingi ya usawa.
Tusipende kuwanufaisha wanasiasa wachache wanaolipwa kufuru!
Premise yako siyo sahihi. Ni kwamba tuwatake wabunge nao walipe kodi kama raia wote, tusiseme kuwa kwa vile wao hawalipi, basi na sisi tusilipe. Wao kutolipa kodi ni kosa, kwa hiyo tusi-expand kosa hilo. Ni lazima viongozi wote, hata rais, walipe kodi kama raia wengine wa jamhuri.
 
Sasa labda nikuongezee tuu kuna jamaa wanaitwa laptop city ukitaka kununua kitu wakati wa ku check out VAT inaongezeka..sasa kimsingi huyu mama anataka watu wa instagram na facebook walipe kodi yani ulipe kodi kwa kutafuta wateja online...🤣🤣🤣🤣 hizo ulizoziwema sijajaribu ila nadhani unaweza kuta mwishoni VAT inaongezeka
Kwanza hiyo imejibu quote post yako iliyoweka kabla ya hii; ni vizuri ungeziunganisha tu.

Kama platform hizo wanalipa kodi, basi hakuna haja ya kupiga kelele; hizo ndizo online businesses. Facebook na Instagram siyo platform za biashara na wala huwezi kusema kuwa hizo ni online businesses; pale kilichopo ni matanganzao tu kama ambavyo mtu angebandika tangazo lake kwenye nguzo ya umeme au angeweka tangazo lake gazetini au redion. Tangazo siyo biashara!
 
Sasa mkuu wewe unadhani huyu mama anazungumzia hizo platform? Yeye huyu anazungumzia facebook na instagram...
 
Si kasingle maza sugu,kazi yake bungeni kuongea pumba tupu kalisema wanaume wameishiwa nguvu za kiume...kumbe kenyewe mbususu bwawa la mtera
Kanatafuta uteuzi haka. Kaache kajishaue kamuuluze yule wa Mbeya aliyetaka kubanana na Betina ambaye ni kinew sabufa. Alichomekewa wahuni akajisahau akanaswa anagawa rushwa sijui kaishia wapi mwizi wa taulo za geust.
 
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi Mheshimiwa Neema amehoji kwa nini biashara za mtandaoni hazitozwi kodi kama biashara nyingine zinazofanyika nje ya mtandao. Mbunge huyo amenukuliwa akisema "Biashara ikifikia mauzo ya 4m, TRA wanatoza Kodi ya 100k/mwaka.

Biashara ikifikia mauzo ya 100m wanasajiliwa VAT na wanatozwa Kodi kulingana na Faida. Kwanini biashara za mtandaoni zisitozwe Kodi hata zikifikia mauzo stahiki? TUJADILI Online vs Offline ✍".

Pia, soma:

1). Dkt. Ndugulile: Kutoza kodi Mapema kwenye Biashara za mitandaoni kutaua ajira za Vijana wengi na kudumaza e-Commerce

View attachment 2145753
Kwani mtu aliye-online si ana offline tayari na analipa kodi, shida nini?
 
Yuko sahihi kabisa; Marekani siku hizi majimbo mengi yanatoza kodi mauzo yote ya mitandaoni. Kampuni kama Amazon, maduka yake ni ya mtandanoni na ndiyo yenye mauzo mengi kuliko kampuni yoyote.

Sasa iwapo wa offline mwenye mauzo kidogo analipa kodi, iweje online mwenye mauzo mengi asilipe kodi.

Tatizo sasa litakuwa kwenye uhakiki wa hizo biashara za mtandaoni
Anauza mtandaoni lakini kupitia biashara grounded na inayolipa kodi
 
Kuna tofauti ya kutafuta wateja mtandaoni na kufanya biashara kwa njia ya mtandao. Watanzania wengi wanatafuta wateja mtandaoni na sio kufanya biashara mtandaoni.

Unakuta mtu ana duka lake Kariakoo na anawapa vijana bidhaa watagute wateja mtandaoni kwa lengo la kuiuza. Kwa mfano huo utasema hiyo ni Online Business?

Ni muhimu kuielewa kwanza dhana ya e-Business kabla ya kufikiria kulipa Kodi.
Exactly my point. Ni sawa na mtu aweke bango kubwa la matangazo barabarani useme anafanya biashara barabarani, anatafuta wateja barabarani tu
 
Sababu hafifu sana hiyo. Mbona unalipishwa tozo wakati bado ni taifa changa wala huduma za kibenki hazijasambaa sana huko vijijini na unalipa.
Na wewe umezingua... Mbona wawekezaji wanapewa tax holiday mpaka five sijui 10 years are they better than us??
Kwakua watz hatuna maamuzi ndo mnatushindilia mamizigo yoote wakati na wao mishahara sijui poshi hazikatwi kodi
 
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi Mheshimiwa Neema amehoji kwa nini biashara za mtandaoni hazitozwi kodi kama biashara nyingine zinazofanyika nje ya mtandao. Mbunge huyo amenukuliwa akisema "Biashara ikifikia mauzo ya 4m, TRA wanatoza Kodi ya 100k/mwaka.

Biashara ikifikia mauzo ya 100m wanasajiliwa VAT na wanatozwa Kodi kulingana na Faida. Kwanini biashara za mtandaoni zisitozwe Kodi hata zikifikia mauzo stahiki? TUJADILI Online vs Offline [emoji871]".

Pia, soma:

1). Dkt. Ndugulile: Kutoza kodi Mapema kwenye Biashara za mitandaoni kutaua ajira za Vijana wengi na kudumaza e-Commerce

View attachment 2145753
Watanzania wengi hawafanyi biashara ya online ni wanatafuta wateja nafikiri mtu anayefaa kutozwa kodi biashara yake iwe imesimama kama wanavyofanya amazon na kikuu
Kumtoza mtu kodi biashara yake anaganyia whatsup status, insta au twitter ni uwonevu
 
Haka kabunge huwa kanajiona kanajua sana mambo kumbe seti tupu. Magu alitukosea sana Watanzania kutujazia ngumbaru bungeni.
Kumbe umekaona....kanajiaminisha eti kapo smart...kumbe kichwani peupe pee...
Watu wanamuangalia tu...
 
Kumbe umekaona....kanajiaminisha eti kapo smart...kumbe kichwani peupe pee...
Watu wanamuangalia tu...
Yaani kajinasibu moja ya wasomi nchini! Huyu angekuwa lile bunge lenyewe la akina Seleli, Lisu, Mwakyembe huu upupu wake anaochangia wala usingekuwa unajadiliwa. Bunge la Kibajaj na Msukuma.
 
Kuna tofauti ya kutafuta wateja mtandaoni na kufanya biashara kwa njia ya mtandao. Watanzania wengi wanatafuta wateja mtandaoni na sio kufanya biashara mtandaoni.

Unakuta mtu ana duka lake Kariakoo na anawapa vijana bidhaa watagute wateja mtandaoni kwa lengo la kuiuza. Kwa mfano huo utasema hiyo ni Online Business?

Ni muhimu kuielewa kwanza dhana ya e-Business kabla ya kufikiria kulipa Kodi.
Umeongea bonge la point mzee.
 
Na huyu naye ni mbunge na yupo ndani ya bunge letu tukufu!
Aisee kweli watanzania tunachezewa kama Midori.
Kwa hili na Kwa mara ya kwanza kabisa,namtupia lawama kipenzi chetu late JPM Kwa kutujazia hii mindondocha bungeni.
 
Nimemwelewa hivyo; angalia juzi nilinunua kitu amazon.com, bado nililipia tax. Vile vile, kwa Amazon kuniuzia kitu mtaani kwangu, serikali ya mtaa nayo inapata kodi ya biashara kutoka Amazon.

Kwa hiyo serikali inapata kodi mbile: ile ya mauzo kutoka kwangu mnunuzi, na kodi ya biashara kutoka Amazon muuzaji, ingawa ile % ya kodi ya biashara ni ndogo sana kwa biashara za online kulinganisha na zile za offline, lakini bado wanalipa.

View attachment 2145767
Tatizo la Tz kodi kubwa 18pc, washushe kodi iwe hata 10pc watu watalipa bila tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja kwa moja kwenye mada.

Kwamba kumeibuka mjadala kwa kusudia la TRA kuanza kutoza Kodi kwa biashara zinazofanyika kwenye mtandao.

Nachojiuliza mimi ni kwamba teknolojia unabadili mbinu za kufanya biashara sasa hivi hili jambo ni la kufanyia mjadala kweli? Hili swala ni kweka tuu kanuni na kuanza kukusanya kodi ya serikali Kwa wahusi.

Watu wanafanya biashara za mabilioni kwa mamilooni afu hamuwatozi Kodi mnahangaika na mageti ya wakulima uchwara.

Serikali wekeni utaratibu mzuri Ili wahusika walipe Kodi kwa sababu Kwa sasa maendeleo ya teknolojia yanabadili mtindo wa ufanyaji biashara..

Nchi nyingi tuu zinatoza Kodi kwenye mitandao na nyingine karibu zinaanza kama Rwanda,huku Tzn mnaendelea kujivutavuta.

Screenshot_20220313-073701.png
 
Back
Top Bottom