Mkuu issue ni kwamba online business Bongo haija-mature kutokana na Utapeli na watu wengi kuwa waoga na bado hakuna friendly facilities za payment gateways ambazo mtu analipa palepale na pesa kuingia kwenye platform Tukichukulia mfano wa platforms kama alibaba au ebay (ambayo inawaunganisha wauzaji na wanunuzi) wote wakiwa wamesajiliwa wale sellers wanafahamika na mauzo yanaeleweka ni rahisi kuwabana kulipa kodi..., na platform as a business pia italipa kodi...,
Tukija huku mfano kama huo labda ni kama KUPATANA au Insta / whatsapp au tangazo humu JF watu wanaongea alafu wanaenda kumalizana wanapojua..., Hence huenda biashara hizo ni ndogo kama mtu kuuza simu yake used, laptop used au hata ya wizi..., au ni maelekezo tu ya kwamba napatikana wapi offline ili mtu anifuate niweze kumlipa nikiwa huko......
Kwahio Serikali isingeharibu kuanzia mwanzo kufanya digital payments kuendelea kuwa affordable huenda watu wengi wauzaji hata wadogo wangeweka option ya malipo online ili yawe tracked (though hata hapo uaminifu na wizi wa wabongo ni wangapi watalipa pesa kabla ya kuona mzigo) ?, Au kama payments zitakuwa na makato makubwa kwanini asimrushie Mmpesa / Tigopesa offline ili wamalizane ?
Utaona kwamba as is with many things nchi hii Serikali inalikoroga kwa uroho wake wa kutaka kuvuna bila kupanda hivyo kupelekea ukuaji wa hizi sekta kusuasua....;
Pia kuna Offline Businesses with Online Presence Na Kama ni kampuni kubwa Online si bado mnunuzi atapata risiti hence kuonyesha mzigo umetoka accordingly (Pia Kampuni zote za Betting, Tickets, Universities n.k.) zinafanya kazi online na zinalipa Kodi accordingly kutokana na kwamba wana mfumo tayari wa payment gateways ambazo bado zinakuwa cheaper na Serikali huko inapata pesa yake husika...