Watu wanaoitwa wakandarasi wa ndani sitaki hata kuwasikia isingekuwa ni haya mambo ya ajili,hili jinamizi la wakandarasi wa ndani ni takataka. Wametuharibia barabaraba zetu. Hata majengo ya hospital,madarasa,madaraja,na kila kitu wanachogusa wao,sio tu chini ya kiwango,bali ni matakataka. Kuna mmoja akatengeneza barabara kubwa tu,inayounganisha wilayala na wilaya nyingine,pia na mkoani,kwa kiwango cha lami. Akatengeneza na barabara ya muda wakati anaendelea kutengeneza kubwa. Hiyo ya muda tulipita kama miezi mitatu hivi tukila vumbi ya kutosha. Watu wakavumilia kwa kujua mterezo unakuja. Bwana ile barabara inafunguliwa ili tuendelee kuitumia wakati anaendelea kumalizia. Watu tunasubiri kitu kiishe,mashimo yakaanza ndani ya miezi mitatu ya kuitumia,watu si wakajua si bado inaendelea kutengenezwa kumbe ndio amemaliza bwana. Watu wakaanza kalele. Jamaa akaona isiwe kesi,wasije kuniua hawa. Akakwapua hela zake serikalini akahama na wilaya. Wengi niliowashuhudia ni chini ya kiwango kupitiliza