Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE NICODEMAS MAGANGA Amesema Trilioni 1.7 ni Bajeti Ndogo kwa Wizara ya Ujenzi, Fedha Iongezwe
"Maeneo ya Kanda ya Ziwa tunayo changamoto, Barabara ni mbaya sana, nyingi ni za vumbi, Magari yanakata Chesesi kwasababu ya ubovu wa Barabara. Bajeti ya Trilioni 1.7 ni ndogo sana, Waziri wa Ujenzi umuombe Mheshimiwa Rais akuongezee fedha" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
"Wilaya ya Mbogwe ambayo ni Mkoa wa Kimadini tumejaliwa kuwa na Madini, Mifigo na Mazao mengine. Tunalo Daraja Mwabomb kila mwaka linasumbua. Naomba ulitengee KM 1 ya lami ili likitengenezwa vizuri liwe linapitika maana ni Barabara ya TANROAD ni ya muhimu sana kwa wananchi iliyounganishwa na Shinyanga na Geita" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
"Lipo daraja la Budoda, naomba Serikali itenge hata nusu KM ili tuondokane na usumbufu kila Mvua zinaponyesha Barabara inakatika wananchi wanateseka. Tuna miaka 61 ya Uhuru, ni vyema tuwe na mtazamo wa haraka kuweza kusaidia wananchi wetu" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
"Kuna daraja la Ilangale na Ikaranga ambayo Wilaya imeunganishwa na Wilaya ya Bukombe. Kila mvua zikinyesha, naomba nusu KM tu na tumetoa mapendekezo Barabara iingie TANROAD ili tuondokane na usumbufu" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
"Kuna mto Nyikonga, kupitia mradi wa Rais tunaenda kutengeneza Barabara ya lami kutoka Nyikonga - Lulembera - Kashero. Naomba mpango uharakishwe haraka mwezi Agosti maana kila kitu kimeshakamilishwa, utekelezaji wake uanze haraka" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
"Mkoa wa Kimadini wa Mbogwe ambao unazalisha dhahabu kwa wingi ukiitoa Geita na Chunya huwa tunapata mali nyingi sana lakini magari yanayotumika yanabeba zaidi ya Tani 30, Sheria za TARURA hairuhusu gari kutembea chini ya Tani 10 kushuka chini" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
"Wafanyabiashara wa Mbogwe wana Malori yanabeba Tani 35. Barabara ya Kanegele - Mpakalimbizi - Segese naomba ipandishwe kuingia TANROAD ili wafanyabiashara wasigombane na watumishi wa TARURA" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
"Ipo Barabara ya Mwalo - Iyogelo - Iponya Masumbwe tumepakana na Wilaya ya Bukombe. Naomba iingizwe TANROAD ili wafanyabiashara wa marudio wanaobeba zaidi ya Tani 30 waweze kuruhusiwa kupitisha magari yao maana mpaka sasa wanapitisha kinyume cha Sheria na huwa wanakamatwa wanapigwa faini" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
"Ipo Barabara ya Bwerwa - Mwendamwizo inatokea Bukori. Kutoka Masumbwe - Lugunga - Makao Makuu Wilaya ya Mbogwe. Barabara hii ni muhimu sana, wenye Malori wanaitumia lakini ipo TARURA hivyo wanazuiliwa wenye magari makubwa kupita. Naomba ichukuliwe kisheria ili wafanyabiashara wafanye biashara vizuri" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
"Masumbwe Mjini nilipata KM 1 ya lami, naomba Waziri wa Ujenzi unisaidie Masumbwe Mjini kuelekea Shule ya Kasandalala naomba KM 1. Makao Makuu ya Wilaya yapo Mbogwe, naomba ipate KM 2 za lami" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
"Wakandarasi wamekuwa wakipata kazi lakini fedha zinachelewa hasa Wakandarasi wa ndani, Waziri wa Ujenzi naomba lifuatilie hili suala maana Wakandarasi wa ndani hawana mitaji, wanategemea fedha kutoka Serikalini ili waendelee kufanya kazi vizuri" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe.