Mbunge Norah Mzeru Apongezwa na Uongozi wa Shule ya Msingi Mahenge B

Mbunge Norah Mzeru Apongezwa na Uongozi wa Shule ya Msingi Mahenge B

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Uongozi wa Shule ya Msingi Mahenge B, Iliyopo Wilaya Ya Ulanga Inapenda Kutoa Shukruni kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mhe. Norah Waziri Mzeru kwa Kuwa Mmoja wa Viongozi ambao Wamechangia kwa Namna Moja Au Nyingine Ujenzi wa Vyumba Viwili vya Madarasa na Ofisi ya Walimu wa Shuleni hapo.

Uongozi umesema kuwa hatua aliyochukua Mbunge Norah Waziri Mzeru ni nzuri kwani imethibitisha ni kwa kiwango gani anaunga Mkono Juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais waJamhuriyaMuunganowaTanzaniaMhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mhe. Norah Waziri Mzeru alichangia Mifuko 50 ya Saruji katika kulianzisha ili kukamilisha jengo la Vyumba Viwili vya Madarasa na Ofisi ya Walimu katika Shule ya Msingi Mahenge B iliyopo Wilaya ya Ulanga ndani ya Kijiji cha Safari Road

Vilevile, Viongozi wa Kijiji cha Safari Road kinaendelea Kuwashukuru Wale wote ambao Wamesababisha Mafanikio ya ujenzi wa Madarasa na Ofisi ya Walimu

#UWT IMARA JESHI LA MAMA
Kazi Inaendelea.

WhatsApp Image 2023-08-28 at 16.52.48.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-28 at 16.52.47.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-28 at 16.52.27.jpeg
 
Back
Top Bottom