Huu uchawa asee yajayo yanafurahisha na kusikitisha kwa wakati mmoja.
====
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Mhe. Nusrat Hanje ameandaa Maombi na Dua Maalum ya Viongozi wa Dini na Wazee kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Tukio hilo linafanyika leo Februari 20, 2025 nyumbani kwa Mbunge Hanje Ikungi, Mkoani Singida, mbali na kumuombea Rais pia inaenda pamoja na kuombea Amani katika Uchaguzi Mkuu 2025
View attachment 3242778
Soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Watanganyika ni wabinafsi sana ndio maana wanatawaliwa kihuni.
Huyo Mbunge haoni future ya watoto wa wengine katika rasilimali za umma.
Yaani watanzania akisha pata pesa anajenga nyumba basi hawazi kuwa nyumba unaoitwa na wakati ,inachakaa na kubaki gofu na kuwa nyumba haina majibu ya Haki za watu.
Ukraine imeingizwa kwenye uharibufu mkubwa na watawala na majeshi yanayopokea amri za kijinga badala ya Kukaa na kutafakari.
Tanzania Kwenye hili la Uchaguzi wa kiini macho unaoandaliwa kwa gharama kubwa wakati wana kura na wapiga kura feki,serikali CCM na tume wasipoangalia na kutafakari na kuepuka tamaa za wanasiasa tutalipasua Taifa letu .
Wetu wanajipendekeza kwa watawala ili wapate vyeo na madaraka bila kujali haki za wengine .
Tumeona hata polisi wakiwa wanaviongoza wanaojali vyeo vyao na nafasi walizonazo bila kujali jeshi kama taasisi inayoundwa na watoto wa maskini wakulima na wafanyakazi wenye ndugu wa vyama tofauti na itikadi tofauti. Wamebaki kuwaza kuwa Bila CCM akuna Serikali . Matokeo yake wanakua kama Jeshi la Ukraine lililotumika vibaya kuharibu nchi yao . Wote sasa hawana makazi Ukraine wala watoto wao wala chama walichokiona ni cha maana bila kutafakari kwa kina. Leo Ukrai imebaki magofu . Kuijenga itachukua mrefu .
Tusipoangalia vizuri kama jamii moja ya watu wamoja wanaostahili kuishi ,kanisa Katoliki lisimama kwenye misingi ya Haki na kuwashauri Waumini wake wote waliopo kwenye jamii ,siasa ,utawala ,tume ya uchaguzi na ndani ya majeshi kwa kiapo kabisa au waislam wa kweli wanamuogopa Allah sio wale wa kusubiri pesa za misaada ya watawala na wageni nao pia waseleme ukweli kwani wasiposimama kwenye ukweli na haki hii nchi itapita katika wakati mbaya na mgumu sana kwa sababu uwezo wa polisi kuua ,kuteka,kupiga ,kujeruhi,kukamata ,kutawanya na hata kufunga wetu ni mkubwa sana kutokana na maandalizi yao uwezo wao n.k. ,Lakini kwenye hili la No Reforms No Election linaweza likaiacha nchi yetu kwenye uhasama mkubwa sana .
Hawa wazanzibar wanatupitisha sisi watanganyika kule waliopita wao .
Tulitegemea Rais Samia angeepusha Wananchi na madhila kama yale waliyoyapata Wazanzibari kwa miaka mingi kutokana na Chaguzi za kihuni. Lakini cha ajabu anataka kuandaa polisi kuzima vyama vingine ili Chama chake kishinde.
Hii ni sawa na Rais wa Ukraine kuamuru jeshi lake kuingia kwenye vita na Urusi bila kujali kuwa atapoteza Raia wangapi na askari wangapi lakini kuharibu kabisa ustawi wa nchi yake .
Ni kweli kubwa Chadema kwa sasa ni chama kikubwa sana na ama kwa uhakika kinaweza kuwa na mashabiki wengi ndani na nje ya nchi. Na wengine wapo ndani ya CCM.
Sasa ni upuuzi mkubwa kuamuru Jeshi la polisi kujiandaa kuua au kujeruhi au kufunga watu ambao wingi wao na familia zao ni karibu nusu ya Watanganyika wote. Hii ni hatari sana.
Samia na IGP wasipotafakari vizuri wataibomoa nchi badala ya kuijenga katika misingi ya Haki. Nchi inajengwa katika misingi ya haki.
Siasa ni suala la sheria na katiba sio suala la tamaa za utawala na vyeo.
Kwa sasa nchi imevamiwa na machawa na wapenda vyeo ili wajinufaishe wanasahau nchi iliharibika hata vyeo vyao havitakua na manufaa kwao pia.