Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. OLIVER AUNGANA NA WANA KAGERA KUMPONGEZA MHE. RAIS NA MKUU WA MKOA KAGERA
Leo, tarehe 30 Novemba 2024, historia imeandikwa katika Mkoa wa Kagera, ambapo wana Kagera walijumuika kwa pamoja kumpa heshima Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake mahiri na juhudi za kuleta maendeleo. Hafla hii ya kipekee ilihusisha maandamano ya amani kuanzia eneo la Rwamishenye Roundabout hadi ukumbi wa shule ya sekondari Bukoba, ikidhihirisha mshikamano wa wananchi na viongozi wa Mkoa wa Kagera.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera, Mhe. Oliver D. Semuguruka, alishiriki kikamilifu katika tukio hili muhimu, akionyesha mshikamano wake na wananchi wa Kagera. Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge Oliver aliwashukuru na kuwapongeza wananchi wa Kagera kwa kushiriki kwa amani na kwa wingi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Aidha, Mheshimiwa Oliver alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Hajat Fatma Mwassa, kwa kazi kubwa ya kuunganisha Mkoa wa Kagera kwa miundombinu bora na kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. Alieleza kwa dhati namna ambavyo Kagera imepiga hatua kubwa chini ya uongozi wa Mhe. Mwassa, akitaja mfano wa utatuzi wa migogoro, maendeleo ya miradi ya kijamii na uwekezaji, pamoja na ushirikiano wa karibu na wananchi wa kada zote.
Pia, Mhe. Oliver alimshukuru kwa dhati Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyoendelea kuipa Kagera kipaumbele kwa miradi mikubwa ya maendeleo kama ujenzi wa barabara, hospitali, shule na miradi mingine ya kimkakati. Alieleza kuwa Rais Samia ameonyesha dhamira ya dhati ya kuimarisha huduma kwa wananchi na kuleta mageuzi chanya katika Mkoa wa Kagera.
Hafla hii iliudhuriwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Cde. Nazir Karamagi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), na Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera. Viongozi wa Serikali, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Katibu Tawala wa Mkoa, na Wakuu wa Wilaya zote za Kagera pia walikuwepo. Zaidi ya hayo, hafla ilipambwa na uwepo wa viongozi wa dini, makundi ya vijana, wanawake, na wadau wengine kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa.
Tukio hili lilikuwa si tu fursa ya kumpongeza Rais na viongozi wa Mkoa wa Kagera, bali pia liliimarisha mshikamano na upendo miongoni mwa wananchi wa Kagera.
Hafla hii ni ushahidi wa mshikamano wa kipekee kati ya wananchi na viongozi wao, na inatoa mwanga wa matumaini kwa maendeleo endelevu ya Kagera na Tanzania kwa ujumla.
Kagera imeahidi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa juhudi za kuijenga Tanzania yenye maendeleo jumuishi na ustawi wa watu wote.
#Samia na Oliver; Kazi Iendelee
#Kagera na Samia
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-11-30 at 17.02.06.jpeg459.6 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 17.03.03.jpeg637 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 17.03.04.jpeg553.6 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 17.05.05.jpeg476 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 17.05.06.jpeg354.5 KB · Views: 3