babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 14,478
- 18,341
Dah huyo bibie hafanani kabisa na hayo mambo,sema na yule dogo kwenye simu kazingua zaidi.Taarifa hii ni kwa mujibu wa Martin Maranja Masese kupitia mtandao wa X, habari ikimuhusu Pauline Gekul.
Kaandika hivi:
"Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul kadhaminiwa polisi Babati, karudi nyumbani kwake kupumzika baada ya kuhojiwa, lakini anasema anahofia usalama wake.. kwani Gekul anatakaje? Tumpelekee chupa za Coca-Cola zimlinde?"
Kabla ya hapo aliandika...
PAULINE GEKUL hadi muda huu saa 20:50 usiku EAT, anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Manyara, pichani akiwa ofisi za RCO - Manyara.
Kamanda wa polisi Manyara, GEORGE KATABANZI amegoma kutoa maelezo ya ziada ya kwanini anashikiliwa, amesisitiza ni taratibu za upelelezi. Taarifa nyingine ni kwamba katibu wa Pauline Gekul anayeitwa HUSSEIN S. ABRIMA na vijana wawili walioshiriki utesaji ule, wanashikiliwa polisi.
Taarifa tulizonazo ni kwamba jalada lililofunguliwa polisi ni malalamiko ya Pauline Gekul kutaka kuuwawa na siyo malalamiko ya Hashimu Philemon.Afande George Katabanzi, tunataka kuona haki ya Hashimu inapatikana polisi. Watanzania tupo tayari kuchanga fedha akapimwe hospitali za kisasa.
Tunakwenda kumpima kupata ushahidi wa kitabibu wa kumuingizia chupa makalioni Hashimu. Mnachelewesha ili ku-buy time eeh? Tumeshtuka.Tutafungua kesi mbili kama hamtaki kumshtaki Pauline GEKUL.
Tutafungua kesi ya jinai, madai na kikatiba na tutaomba tafsiri ya mahakama kuu.Tunao mawakili wa kutosha. Jopo linaongozwa Manyara na Wakili Thadei, Wakili Madeleka na mawakili wengine. Hatutaki kona-kona katika hili.
Pia soma >>>
1. Mbunge Pauline Gekul Akamatwa na Jeshi la Polisi Akijaribu Kutoroka Nchini Kuelekea nchini Kenya
2. Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto