Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Baada ya kusambaa kwa taarifa ya kuchomwa moto nyumba ya mwananchi wa Mtaa wa Maisaka kati Mbunge wa jimbo la Babati Mjini Mhe Pauline Gekul amejitokeza kuifariji familia ya mwananchi huyo, na kuwasihi wadau wenye mapenzi mema kuendelea kumsaidia muhanga wa tukio hilo.
Akizungumza na mwananchi huyo Mhe Gekul amesema amesikitishwa na tukio hilo, nakutoa mkono wa pole huku akiahidi kusimamia michongo mbalimbali ya wadau inayochangishwa kwa lengo la kumjengea nyumba ya mwananchi huyo.