Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE ROSE CYPRIAN TWEVE Akichangia Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
"Nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuwa Imara na mwanamke ambaye hajatikisika kuhakikisha anaendelea kuliongoza Taifa hili. Nampongeza Mhe. Mwigulu na Mhe. Mkumbo kwa namna ambavyo mnaendelea kumsaidia Mheshimiwa Rais" - Mhe. Rose Cyprian Tweve, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa
"Mhe. Mwigulu wakati anasoma bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 alinigusa sana pale ambapo tunapoteza watanzania wengi kwa viti ambavyo tunaweza kuvizuia (Control) maana viko ndani ya uwezo wetu. Nasikitishwa sana pale kama Taifa tunakuwa na uwezo wa kuzuia vifo vya watanzania lakini hatufanyi hivyo"
"Kila mwaka tunapoteza zaidi ya watanzania 1,500. Ndani ya miaka mitano tumepoteza watanzania zaidi ya 7,000. Naipongeza Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambayo imeliona jambo hili na walisikitishwa na jambo hili. Mwaka 2009 - 2015 walichukua juhudi za makusudi wakatenga zaidi ya Dollar Milioni 48, pesa za walipa kodi, pesa za watu Masikini wakajenga kiwanda cha Viuwadudu pale Kibaha kuhakikisha tunazalisha dawa na kuzipeleka kwenye maeneo yetu kuhakikisha tunatokomeza Malaria nchini"
"Kiwanda cha Viuwadudu, Kibaha ni cha kipekee, tuna viwanda kama hivi vitatu tu Duniani (Japan, Tanzania na Cuba). Kiwanda hiki kinatumia Biotechnology ambayo bidhaa hii haina madhara kwa binadamu, wanyama na mimea. NIMR walitoa hati kuwa dawa inayozalishwa Kibaha ni salama na Safi kwa matumizi ya binadamu"
"Taarifa iliyokuja Bungeni wiki iliyopita toka mwaka 2017 - 2024 tumenunua Lita Laki 190,000 tu ndani ya miaka sita. Uwezo wa kiwanda cha Kibaha ni kuzalisha Lita Milioni 6"
"Wakati tunaweka mikakati tulisema ndani ya miaka mitano ni Lita Milioni 30 tungezalisha na kutokomeza Malaria kwenye Taifa hili, tungeokoa maisha ya watoto, akina mama na nguvu kazi ambayo ingekuja kufanya kazi kupandisha Taifa hili"
"Hatuna sababu kuendelea kushuhudia watanzania wakiendelea kuteketea. Mhe. Mwigulu kama ambavyo umekasirishwa na vifo vinavyotokana na ajali, vivyo hivyo tukahakikishe tunapambana kuokoa maisha ya watanzania yanayopotea kwasababu tu hatujatekeleza majukumu yetu"
"Kila mwaka tunatumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kununua Net, kufanya makongamano na kufanya semina. Kama tunatumia Shilingi Bilioni 100 kwenye Semina, ununuzi wa Net na kufanya makongamano, kwanini nguvu hiyo hiyo tusiitumie kuua dawa ya Viuwadudu?"
"Mnatuambia Bungeni ndani ya miaka 5,6 tumenunua Lita Laki 2 na nchi zingine wanakuja kununua dawa kwenda kutokomeza Malaria kwenye nchi yao. Naomba Serikali twende tukakae Kamati ya Bajeti, Wizara ya Afya na TAMISEMI twende kuokoa maisha ya watanzania"
"Nimepitia Bajeti ya Wizara ya Afya, wametaka Malaria mara 57 lakini hakuna kifungu kinachosema tunaenda kununua dawa na kutokomeza. Tunatumia neno mapambano dhidi ya Malaria, tunapambana na nini? Kiwanda kipo Kibaha ni kununua dawa na kunyunyizia, hayo mapambano tuyapeleke kwenye magonjwa yanayoshindwa kutibika" - Mhe. Rose Cyprian Tweve, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa