Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge Sebastian Kapufi: Tanzania ๐น๐ฟ kwa ujumla wake tuna Wakia Milioni 45 ya akiba ya dhahabu lakini leo tunasomeka ni kati ya nchi Masikini Duniani
"Hotuba ya Waziri Mkuu Imezungumzia Maji, Misitu, Madini, Kilimo. Kuna Nchi Haina Msitu ni Jangwa. Kwa Nchi Yetu ya Tanzania ๐น๐ฟ Kila Kitu Kipo, Kwanini Tunaangukia Kwenye Nchi Masikini, Ni Wapi Tumekosea?" - Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini
"Namshukuru Mama Samia. Pale kwetu Katavi kulikuwa na shida kubwa ya Suala la uchujaji damu kwenye Figo. Wapiga kura wamehamia Mbeya, Dar es Salaam, Mwanza kwaajili ya Suala la uchujaji damu kwenye Figo maana kwa Wiki moja alikuwa anachuja damu mara tatu, hawezi kukaa Mpanda" - Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini
"Mama Samia Suluhu Hassan amenileteq fedha Mpanda kwa kuanzia Shilingi Milioni 196 kwaajili ya kujenga chumba cha kusaidia wagonjwa wa uchujaji wa damu. Ule mradi kwa ujumla wake ni Shilingi Milioni 400. Nashukuru sana katika hilo" - Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini
"Skimu ya umwagiliaji maji ya Mwamkuru tumeletewa Shilingi Bilioni 31, Skimu kasi yake ni ndogo lakini naomba Wataalam waongeze kasi. Tuna mradi wa TACTIC ulikuwa na shida kidogo lakini Wataalam wamefanya utafiti tuna kilomita 8.2 za lami kwaajili ya Mji wa Mpanda na miji 28 kutatuliwa tatizo la maji katika mji wa Mpanda" - Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini
"Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kuna fidia kwa wananchi wa Bwawa la Mirara na fidia ya wananchi waliopisha ujenzi wa barabara kutoka Starike kuja Mpanda Mjini. Tunaomba sana fidia ya maeneo hayo" - Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini.
"Biashara ya Kaboni (Misitu na Uoteshaji Misitu) ni chanzo kikubwa cha mapato. Tunapotengeneza Madampo ya kisasa tufikirie kuhusu Biashara ya Kaboni. Kamati tulishauri elimu ya Kaboni iwafikie wabunge wote" - Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini.
"Miradi ya Barabara, Reli, Viwanja vya Ndege na Bandari. Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma - Tabora - Mwanza - Kigoma ni jambo jema sana lakini kipande cha Kaliua - Mpanda - Karema kisomeke. Kutoka Mpanda - Dar es Salaam kwa Treni ya kawaida ni siku tatu, kwa Ndege ni masaa mawili. Katika hili Naishukuru Serikali" - Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini.
"Ghana ๐ฌ๐ญ ni ya kwanza kwa uzalishaji dhahabu Africa ๐ inazalisha Tani 117. Tanzania ๐น๐ฟ inashika nafasi ya Nne kwa uzalishaji. Duniani; China ๐จ๐ณ (370 Metric Tons), Australia ๐ฆ๐บ (310 Metric Tons), Russia ๐ท๐บ (310 Metric Tons), Canada ๐จ๐ฆ (200 Metric Tons) na United States of America ๐บ๐ธ (170 Metric Tons).