PreGE2025 Mbunge Suma Fyandomo achangia Milioni 374.5 miaka mitano ya Ubunge, UWT Mkoa wa Mbeya wampongeza sana

PreGE2025 Mbunge Suma Fyandomo achangia Milioni 374.5 miaka mitano ya Ubunge, UWT Mkoa wa Mbeya wampongeza sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhe. Suma Ikenda Fyandomo amewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Mbunge kwa kipindi cha miaka mitano (2020-2025) katika kikao cha Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Mbeya

Suma Ikenda Fyandomo amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya Ubunge amechangia michango ya takribani shilingi Milioni 374.5 (374,500,000) kwaajili ya Kuwezesha shughuli mbalimbali za Chama (CCM), Jumuiya za CCM (UWT, UVCCM na Wazazi) na Serikali.

Aidha, Suma Ikenda Fyandomo aliwasilisha Taarifa yake ikionyesha mchango wake katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye Afya, Elimu, Miundombinu, Maji, Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi. Pia, Kazi alizofanya Bungeni, Kazi alizofanya kwa kushirikiana na Taasisi zingine na kazi alizofanya kufanikisha shughuli mbalimbali za CCM.

"Kati ya Wanawake 44 waliogombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya mwaka 2020 mliniona na kunichagua. Nawashukuru sana kwa kunituma. Na sasa naomba mnitume tena nikawawakilishe Bungeni kwa awamu ya pili (2025-2030)" - Alisema Suma Ikenda Fyandomo

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Vilevile, Suma Ikenda Fyandomo wakati akiwasilisha Taarifa yake mbele ya Baraza la UWT Mkoa wa Mbeya, alichangia Madirisha ya Aluminium kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa Hosteli ambao ni mradi wa UWT Mkoa wa Mbeya

Mwisho: Viongozi wa UWT Mkoa wa Mbeya wamemshukuru na kumpongeza sana Mhe. Suma Ikenda Fyandomo kwa kazi nzuri na kazi kubwa ambayo ameifanya kwa kipindi cha miaka mitano ya Ubunge 2020-2025 na kumtakia kila la heri na kusema wamemuona akishirikiana nao katika shughuli zote kwa moyo bila kusita.

WhatsApp Image 2025-06-25 at 06.00.39.jpeg
WhatsApp Image 2025-06-25 at 06.00.43.jpeg
WhatsApp Image 2025-06-25 at 06.00.41.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-06-25 at 06.00.40.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-25 at 06.00.40.jpeg
    115.2 KB · Views: 38
  • WhatsApp Image 2025-06-25 at 06.00.43 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-25 at 06.00.43 (1).jpeg
    110.5 KB · Views: 39
  • WhatsApp Image 2025-06-25 at 06.00.43 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-25 at 06.00.43 (2).jpeg
    100.2 KB · Views: 39
  • WhatsApp Image 2025-06-25 at 06.00.44.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-25 at 06.00.44.jpeg
    84.6 KB · Views: 38
Back
Top Bottom