PreGE2025 Mbunge Tauhida Gallos na Miaka Mitano (2020 - 2025) ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM

PreGE2025 Mbunge Tauhida Gallos na Miaka Mitano (2020 - 2025) ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi, Kichama, Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo tarehe 11 Mei, 2025 amewasilisha ripoti ya Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Mbunge kwa kipindi cha miaka mitano (2021 - 2025) katikap ukumbi wa Uwanja wa Ndege SACCOS uliopo Wilaya ya Magharibi B.
WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.36.jpeg
Mhe. Tauhida Gallos amewasilisha taarifa hiyo mbele ya Katibu wa Kamati Maalum, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Khamis Mbeto Khamis ambaye amewataka viongozi kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo ili kuendelea kukipa sifa Chama (CCM)
WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.42.jpeg
Katika hotuba yake akizungumza na UWT Mkoa wa Magharibi, Ndugu Khamis Mbeto Khamis Amesema ili kuwa kiongozi bora ni lazima kushuka chini, kuanzia ngazi ya shina na kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyafanyia kazi

Aidha, Ndugu Khamis Mbeto Khamis amesema taarifa ya ripoti iliyowasilishwa na Mbunge Mhe. Tauhida Gallos imeonyesha wazi kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa magharibi kimefanya mambo makubwa kwa kuhakikisha wanatatua baadhi ya matatizo yanayowakabili wananchi.

Pia, Ndugu Khamis Mbeto Khamis amewasisitiza Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Magharibi, kuhakikisha wanaendelea kukipigania na kukisimamia Chama (CCM) ili kuendelea kubaki madarakani.

Akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha miaka mitano, 2020-2025 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi, Kichama, Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo amesema katika kuimarisha Chama kwa kipindi cha miaka mitano amefanya shughuli mbalimbali ambazo zimeorodheshwa kwenye taarifa hiyo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mhe. Tauhida Gallos ameainisha miongoni mwa shughuli alizofanya ambazo ni pamona na Kutembelea miradi na kusaidia vikundi mbalimbali ikiwemo kukabidhi kifusi na Saruji (Ujenzi), Jezi (Michezo) pamoja na mahitaji mengine ili kuhakikisha anaendelea kujenga Chama katika ngazi zote.

Naye, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi kichama, Fatma Ameir amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kusimama mstari moja katika kukisimamia Chama ili kuendelea kupata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.41.jpeg
Katika hafla hiyo, Mbunge Mhe. Tauhida Gallos amekabidhi fedha taslimu kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za kiofisi, vitendea kazi pamoja na kumpatia cheti cha shukurani cha utendaji kazi kwa Katibu wake ndugu. Lucy Edward.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.40.jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.40.jpeg
    107.7 KB · Views: 37
Viti maalum ni mzigo mwingine wa walipa kodi wa Tanzania
 
JPM alitoa wapi hawa wabunge empty headed!! Huyu kwenye nchi serious hakupaswa kuwa hata mjumbe wa nyumba 10 ila hapa anaitwa mheshimiwa!! So sad
 
Back
Top Bottom