Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. TIMOTHEO MNZAVA AJIKITA KUTATUA KERO ZA WANANCHI WA KOROGWE VIJIJINI
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava ameendelea na ziara yake ya kimkakati katika jimbo lake huku akijikita katika kuzungumza na wananchi ili kujua changamoto na kuweza kuzitatua.
Mhe. Timotheo Mnzava tarehe 25 Machi, 2023 aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Jokate Mwegelo kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwetonge Kata ya Mashewa juu ya kuanza kwa mradi wa Maji wa Kijiji hicho.
Viongozi wa Vijiji, Kata, Halmashauri ya Korogwe na Wilaya ya Korogwe pamoja na Wana Kwetonge walishuhudia Makabidhiano ya eneo la Kazi kati ya Mkandarasi wa mradi wa maji na RUWASA.
Aidha, Mhe. Mnzava aliendelea na ziara yake na kuzungumza na wananchi wa Kijungumoto, Kwetonge na Magoma. Pia, wananchi wa Kata ya Lewa, Kijiji cha Lewa ambapo waliweza kujadiliana changamoto zilizopo na kutafuta majawabu.
Vilevile, Mhe. Mnzava Jumapili Machi 26, 2023 alishiriki Ibada na Waumini wa Kanisa la Anglican Kwamzindawa na Kanisa la KKKT Usharika wa Hale ambapo alifanya ziara kwenye Vijiji vya Kwamzindawa, Shamba kapori ( Kata ya Mnyuzi) na Kijiji cha Ngomeni Kata ya Hale.