Mbunge wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuangalia uwezekano kuvirejesha viwanda vya mkoa huo ili kuchochea ajira na maendeleo ya kiuchumi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Februari 28, 2025 katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga, wakati wa ziara ya Rais Samia mkoani humo, Ummy amesema kuwa miaka ya 1970 na 1980, mkoa huo ulikuwa miongoni mwa mikoa yenye viwanda vingi nchini, ukiwa wa pili baada ya Dar es Salaam.
"Mama tunakuomba utubebe, utushike mkono tufufue viwanda vya Tanga - kiwanda cha chuma, kiwanda cha mbolea, kiwanda cha saruji, kiwanda cha mablanketi na nguo, pamoja na viwanda vya sisal. Vijana wetu, kina baba na kina mama watapata ajira," amesema Ummy.
Mbali na viwanda, Ummy amesisitiza umuhimu wa jiji la Tanga kuwa na chuo kikuu, akieleza kuwa ni miongoni mwa majiji machache nchini yasiyokuwa na taasisi ya elimu ya juu.
"Tulikuwa tunajenga chuo kikuu Tanga, lakini bahati mbaya kikapelekwa wilaya nyingine. Mheshimiwa Rais, Makao Makuu ya Mkoa yanapaswa kuwa na chuo kikuu. Tunapendekeza kiitwe Chuo Kikuu cha Shaaban Robert, ili kuenzi heshima ya mzee wetu wa Tanga," ameongeza.
Tangu mbunge kombo mpaka ummy wanaomba viwanda virejeshwe huyo anaye omba ndio walioviuza ni nani wa kurudisha pesa walizonunulia ni maneno ya kisiasa kuwa naye alisema kitu!