Interested Observer
JF-Expert Member
- Mar 27, 2006
- 3,384
- 4,428
Unapongeza Rais Kwa kukupa haki yako? Only in a Banana RepublicMbunge wa Viti Maalumu, Esther Matiko amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo aliyoikuta pamoja na kuanzisha miradi mipya huku akipendekeza maslahi ya askari magereza yaboreshwe.
Hayo ameyasema leo Alhamis Juni 22, 2023 wakati akichangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024, jijini Dodoma.
Matiko amesema kasi ya upelekaji fedha kwenye miradi hiyo ya kimkakati ikiwemo kwenye sekta ya nishati, afya, elimu, maji na miundombinu inashawishi wananchi kulipa kodi.
Matiko pia amelilia maslahi kwa askari magereza akipendekeza yaboreshe kama ilivyo kwa askari wa vikosi vingine vya hapa nchini ikiwemo mishahara na upandishaji wa vyeo.
Hiyo ni haki yako