Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Vituko na vibwanga vya wanasiasa vinazidi kuendelea. Huyu mbunge wa viti maalum akiwa na wanachama wengine wameonyesha ushamba na uchawa wa pro max katika kuomba kura.
Nipo pale mbele naendelea kushuhudia vituko vya karne
===============
Katika kipindi hiki cha kampeni za Urais, Ubunge na Udiwani nchini, Mbunge Mteule wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani Msongozi, ametembelea masoko ya Bombambili na Mfaranyaki yaliyopo katika Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, tarehe 19 Septemba 2025.
Katika ziara hiyo, Mhe. Msongozi alikutana na wafanyabiashara wadogo wa masoko hayo na kuwaomba waiunge mkono na kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Akizungumza na wafanyabiashara hao, Mhe. Msongozi alisema kuwa mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kutoa Shilingi bilioni 200 ndani ya siku 100 za kwanza za utawala wake iwapo atachaguliwa, fedha ambazo zinalenga kuboresha mitaji kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini. Hivyo, aliwasihi wafanyabiashara hao kukichagua chama hicho ili waweze kunufaika na fursa hiyo ya mitaji.