Selous
JF-Expert Member
- Jan 13, 2008
- 1,325
- 145
Heshima kwenu wanjamvi,
Ni kweli Mbunge wa Arusha Mheshimiwa Godbless Lema kapigwa sana na polisi [FFU].
Jana iliamuliwa kikao cha kumchagua Meya wa Jiji la Arusha kifanyike leo saa 3 asubuhi,kikao cha jana kilishindwa kumchagua Meya kwasababu CCM walitaka kumchomeeka mjumbe kutoka Tanga ili kuwasaidia kwenye mchakato wa kupiga kura pamoja na mizengwe ya kumchomeka mjumbe wa Tanga lakini bado CHADEMA walikuwa na nafasi ya kushinda kwakuwa diwani wa TLP Mheshimiwa Kivuyo alikuwa akiwaunga mkono CHADEMA.
Maajabu yalianza kujitokeza hiyo saa 3 asubuhi badala ya wajumbe wa CHADEMA kwenda kwenye kikao cha kumchagua Meya waliamua kufanya kikao Hotel Ikweta mkabala na ukumbi wa manispaa ya Arusha.Mheshimiwa Kivuyo baada ya kuona wajumbe wa CHADEMA hawaingii kwenye mkutano aliamua kuwafuata Ikweta Hotel kuwasihi wahudhurie kwenye kikao kwakuwa bado walikuwa na nafasi ya kushinda kiti cha umeya lakini juhudi zake hazikuzaa matunda wajumbe wa CHADEMA waliendelea kususia kikao cha uchaguzi wa Meya.
Mwenyekiti wa kikao cha uchaguzi wa Meya Bwana E Chang'ah aliamua kufanya mawasiliano na ofisi ya waziri mkuu.Waziri wa nchi Tawala za mikoa na serekali za mitaa alitoa maagizo sheria zifuatwe kwa kuwa idadi ya wajumbe ilifikia nusu mchakato wa uchaguzi ukaendela bila ya wajumbe wa CHADEMA kushiriki kwenye kikao.Wajumbe wa CHADEMA wakajulishwa Meya tayari kachaguliwa wakaamua kuingia kwenye kikao wakiongozwa na Mheshimiwa Mbunge G Lema.Zilitokea purukushani za hapa na pale Lema akachomoa bastola FFU wakmvamia na kumpokonya na kumpiga vibaya sana.
Wanajamvi CHADEMA hawakuwa na sababu za kutoingia ndani ya kikao cha uchaguzi wa Meya.Meya alipochaguliwa wajumbe wa CHADEMA wakaamua kuingia sijui waliingia kufanya nini ?.Lema hakutakiwa kutoa bastola yake wakati askari wa usalama walikuwepo eneo la tukio sijui alitaka kumpiga nani ?.Ikumbukwe Lema ana kesi ya kutishia kuuwa Mkurugenzi wa Jiji.
Ngongo,
Nashukuru kwa taarifa hii mana imejibu baadhi ya maswali. Unaweza kumpata mmoja wa madiwani wa CDM wakaelezea sababu?
Hili la Lema kuwa na kesi ya kutishia hailalalishi kutotoa bastola, something is not right here mana wangemnyang'anya tu basi sio mpaka kumpiga.
Alhaji ANS