Ni budi Watanzania tuwaambie polisi kuwa imetosha, hawawezi kuendelea kutumika na CCM kama chombo cha kugandamiza Raia. Vyama vya Siasa, wanaharakati, wasomi, na wananchi wote wenye mapenzi mema, kwa vitendo kama hivi tutoe kauli kuwa adui mkubwa wa haki ya Mtanzania ni CCM na polisi. Kila mahali watu watakapoiona CCM na polisi na viashiria vyake wajue wamemwona adui yao. Hata bila ya kufanya chochote, bila ya kufanya vurugu, hiyo itaosha. Hatuwezi kuwazuia kufanya uovu lakini hawawezi kutulazimisha kuwapa ushirikiano wa aina yeyote.
Kama serikali haiwezi kuchukua hatua dhidi ya polisi hao, na tuna uhakika kuwa mfumo wetu wa mahakama hauwezi kutenda haki, basi matukio haya na yanayofanana nayo yaanze kuchukuliwa ushahidi wa kutosha, na mashtaka yafunguliwe kwenye mahakama ya kimataifa dhidi ya Rais kwa kutumia vibaya vyombo vya dola na kushindwa kulinda haki ya Raia wote kwa haki.